Kwenu wanaume ...Hii imekaaje ?

FirstLady1

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2009
Posts
16,789
Reaction score
5,401
Rafiki yangu mmoja kanijia jana akiwa mwingi wa mawazo na majonzi tele
Kisa nini..Ni mwaka wa tatu sasa ameolewa hana mtoto ,Mama mkwe kapiga simu saa tano usiku kwa mwanae wakiwa wamelala
anauliza mkeo yuko hapo ? jamaa kasema ndio ..basi akaambiwa weka loud spika ili huyo anayejiita mkeo apate vidonge vyake
Mama mkwe bila haya kaanza kuporomosha mvua ya maneno akilalamika kama hajaolewa kuja kumchuna mtoto wao wamemsomesha ili awatunze wao na sisi yeye mke mgumba ..
Mbaya zaidi anamwambia ..hajaolewa ili awe sanamu ndani ya nyumba ..la sivyo wangenunua sanamu wakaweka ndani wanachotaka amzalie watoto kama hawezi njia iko wazi aondoke ..!
Mke kulalamika kwa mmewe ..
Mme anamjibu hii ni message send ..
Wanaume kwa nn mnaruhusu ndoa iingliwe na ndugu mke anyanyaswe kiivyo ?
kwa nini msitoe suport ili mke awe na uwezo wa kujitetea?
shock!!!!
FL
 
mwanaume ameonyesha udhaifu mkubwa sana!
 
.......Mhh inasikitisha kwa kweli, ndugu nao kuingilia ndoa za watu..........hawajui watu wamepanga nini kwenye ndoa zao.Wengine wanatafuta maisha kwanza mtoto baadaye.Miaka 3 mbona michache sana kumsema mdada wa watu?
 
mwanaume ameonyesha udhaifu mkubwa sana!
Udhaifu mkubwa nimefedheheka na hili Geoff

tena na wewe unaenda kuoa wewe kuwa makini sana ! nitawasiliana na ww
 
mwanaume kakosea, mama nae kakosea kwamba alimsomesha ili awasaidie, lakini mtoto muhimu, kama mbinu za utabibu hazijafanikwa na mwanume ana uhakika yuko safi, basi aoe mke wa pili na asithubutu kumfukuza au kumdharau huyu wa sasa kwani si kosa lake

kama mume ndiye mwenye kasoro na anataka watoto, wakubaliane na mama atafute seengeti boyz anayejiheshimu amsaidie kufanya kazi na wasije kumwambia huyo srengeti boyz wala watoto, iwe siri yao hadi kufa
 
Alafu miaka mitatu tu??? Hao ndugu ni wakorofi by nature!! Mbona bado sana, watu wanapata mtt hata baada ya miaka kumi!! Mwanaume dhaifu na mmbea pia, kwann anaruhusu kuweka loud speaker mama yake atukane?? Walikuwa washaongea mchana hao na uyo mwanaume keshaanza plan zake mana subira hapo haipo tena!!
 
.......Mhh inasikitisha kwa kweli, ndugu nao kuingilia ndoa za watu..........hawajui watu wamepanga nini kwenye ndoa zao.Wengine wanatafuta maisha kwanza mtoto baadaye.Miaka 3 mbona michache sana kumsema mdada wa watu?

Pretty mbaya zaidi wanapewa suport na hawa waune zetu ..kama mme angekuwa na msimamo mama asingediriki kupiga simu na kuporomosha maneno makali na mwanae akiwepo!
 

Sina kawaida ya kuchangia mada asubuhi asubuhi jinsi hii ila hii mada imenigusa pahala pabaya.Kwanza nimpe pole huyo shoga yako, pia nimtie moyo kuwa ndoa ni safari isiyopimika!Lakini kubwa kwa hayo mawili ni jamaa yangu ,kaka yangu huyu,Ajue kuitwa mwanaume ni nini hasa, siyo kuvaa suruali na kutoka asubuhi kwenda barabarani kutafuta maisha!Ni zaidi ya hapo!!!Unapomwacha mama yako mzazi asimamie nyumba yako kwa maana ya ndoa ni kwamba siku atakuwa hayupo na ndoa yako haitakuwepo tena.Lakini ustaarabu vile vile unadai heshima hata kama asingekuwa mkeo wa ndoa ni rafiki au hata ndugu kumwekea loud speaker mama yako na kisha akaporomosha matusi na wewe kuitikia msg sent! Inaeleweka upstairs yako haijakamilika hata sekunde moja.Wewe ni kiongozi gani wa nyumba inayoongozwa kwa simu kutoka kwa mama yako?Ulipokutana na huyo mkeo ulimshirikisha mama yako ?Si ulimpenda mwenyewe ?Sasa iweje kupokea ushauri na madhalalisho ya mkeo kutoka kwa mamako nawe kuafiki na kumrushia madongo mkeo?ACHA HIZO.Mshauri huyo shoga yako awe mvumilivu na ampe darasa mumeye huyo.
 
Huwenda mwanaume ndo kasuka hou mpango mzima haiwezekani umjibu mwenzio meseji sent- manyanyaso mengine? FL1 Huyo rafiki yako wameshakwenda kucheck hospital yeye na mumewe kama hawana tatizo lolote?
 

Very wrong move hio.

Inaonyesha wazi ni 'mama's boy' huyo. Once you get married hio
department ni yenu nyie wawili na hizi kochokocho za kutoka kwa
wakwe are uncalled for. Kama namana gani vipi go back to your mother
ukazidi kunyonya!

Very unfair to the lady na pole yangu kwake.

To the mother in law...Get a life!!!!
 
HIVI WEWE,
mchango wetu vipi?....πŸ˜€

G mie ndo dadaako kwanini nikuangushe ..leo au kesho natuma mtu akuwezeshe kazi yangu ya umesenja boss atanimwaga nikitoka kwa ofisi ..

Turudi kwenye mada πŸ˜‰
 
G mie ndo dadaako kwanini nikuangushe ..leo au kesho natuma mtu akuwezeshe kazi yangu ya umesenja boss atanimwaga nikitoka kwa ofisi ..

Turudi kwenye mada πŸ˜‰
mara mama nitilie,mara mesenja!...lol!sijui lini utaniambia wewe ni mama salma...!haya bwanaπŸ˜€
 
hapo kwenye red umenifurahisha Twandefiki ..uko sawa kabisa huyu mwanaume ni dhaifu
 



Jmani nadhani hii ni mbaya sana.Lakini haya yote ni kukosekana kwa umakini wa mwanaume.Haiingii akilini mwanamke atukanwe mbele yako kwani hata wewe mwanaume unaonekana kituko.Mtu anapotukana au kudharau kile ulichokichagua ni sawa na kwamba amekudharau wewe uliyechagua.
 
Huwenda mwanaume ndo kasuka hou mpango mzima haiwezekani umjibu mwenzio meseji sent- manyanyaso mengine? FL1 Huyo rafiki yako wameshakwenda kucheck hospital yeye na mumewe kama hawana tatizo lolote?

Mie pia nimemuuliza swali kama lako yeye kasema alishapima DR akamwambia hana tatizo ila huyu mmewe ndo kila akimwambia akapime hatoi majibu sahihi ..na kudai tayari alishazaa mtoto mwingine nje kabla hajaoa
 

ni sawa kabisa kwenye ndoa kuna kipindi cha mpito siku zote si mteremko
Thanks ABEDNEGO ..
Lakini je huyu mwanamme kuna uwezekano wa kubadilika kama tayari mama mkwe kishatia sumu ndoa yake?
 
hapo kwenye red umenifurahisha Twandefiki ..uko sawa kabisa huyu mwanaume ni dhaifu


FL1, nimepandwa na hasira ya kuua mtu. Huyo boy (wala siyo mwanaume) siyo tu kwamba dhaifu bali ni "mpumbavu mkubwa". Mama yake anaweza kuwa na makosa ila nafasi ya kufanya huo upuuzi anapewa na huyo kilaza wake. Kwani kama ana shida ya mtoto amechukua hatua gani (medically) kuhakikisha kuwa mwanamke ndiye hawezi kuzaa? Na kama hawezi kuzaa walikuwa na makubaliano gani kabla ya ndoa kwamba endapo hataweza kuzaa (kwa mfano) ndoa inakufa? Naanza kushawishika kuwa jamaa anaweza kuwa anajua mapungufu yake na sasa anatafuta upenyo wa kuficha aibu. Si ajabu sperm count zake ni zero na sasa anamtumia mama yake kumtimua huyo dada wa watu ili siri isijefichuka!
 
Mie pia nimemuuliza swali kama lako yeye kasema alishapima DR akamwambia hana tatizo ila huyu mmewe ndo kila akimwambia akapime hatoi majibu sahihi ..na kudai tayari alishazaa mtoto mwingine nje kabla hajaoa

Kwa manyanyaso hayo aombe MUNGU ingawa siku hizi wengi wetu hatuamini saaaana katika miujiza but MUNGU anafanya miujiza. But ningekuwa mimi ningeondoka hapo nyumbani na kwenda kwetu kwana ili nitoe nafasi kama atakavyo mama mkwe. Ningebaki tu kama mume wangu angeonyesha yuko upande wangu.

Kuna rafiki yangu mie alikumbwa na msukosuko kama huo na mbaya zaidi yeye alishambuliwa na familia nzima ya mume na mumewe akiwa ndie kiongozi wao- akamletea mwanamke mwingine aliyedai ana mimba yake. Rafiki yangu akafungasha akaanza mbele na maisha yake. Ameolewa na ana watoto 2 mapacha na yule bwana akaambulia kulea mimba ya mwarabu alipokwenda hospital akaambiwa yeye hana uwezo wa kutungisha mwanamke mimba.

Sasa hivi anamdai mkewe wa kwanza toka kwa mume mwenzie!
 
FL1 na huyo mama nadhani ni wale akina mama waliokosa aibu na busara. Kama aliona kuwa miaka 3 ni mingi kwa mkwewe kutozaa alitakiwa yeye kama mwanamke mwenzie na mzazi awe karibu nae na kumshauri na kumpa moyo kwani ni jambo ambalo hata yeye wakati anaolewa (kama aliolewa) lingemtokea tu. Na kama ni mzazi hao wote ni kama watoto wake wote so issue sio kama kuna tatizo atumie simu tena usiku kwa kuweka loud speaker....Jamaa ana hasara hana mama. abaki na mkewe kivyao iko siku mungu atawakumbuka huyo dada atazaa sijui huyo mama ataenda kuona mjukuu au vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…