Kwenu watia nia, hasa wale wa Urais

Kwenu watia nia, hasa wale wa Urais

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Ushauri huu wa bure ungefaa kuwafikia watia nia na hasa wale wa urais kwani wajumbe wenye kushikilia hatima zao kwenye hili ni sisi.

"Sisi," Watanzania ambao pia ni binadamu kama alivyo binadamu mwingine yeyote wakiwamo pia wao.

Ieleweke wazi kuwa, kwa hulka tu, hayupo binadamu awaye yote anayependa kuishi katika jamii au mazingira yenye kuendekeza:

1. Uongo, janja janja, hadaa, hiana, chuki, ghilba, nk, hasa hasa kutokea kwa mamlaka.

Kukosekana kwa uwazi na ukweli kutoka kwa mamlaka kwa sababu zozote zile ni jambo lisilokubalika asilani.

2. Ukosefu wa haki, uhuru, amani, nk kwa wananchi kutoka kwa mamlaka au mamlaka kushindwa kudhibiti haya.

3. Kutokuwepo kwa demokrasia. Kuwepo kwa tofauti za mawazo hakuwezi kuhalilisha wengine kuwa ni maadui. Kuhalilisha kuuwawa, kupotezwa, kufungwa, kunyanyaswa, kupuuzwa, kubagazwa, nk, kwao.

4. Kutokuwapo na usawa kijamii na hata mbele za sheria (impunity). "Yaani mkuki kwa nguruwe." Haya hayakubaliki.

Na mengine mengi ya namna hiyo ambayo kimsingi ndiyo haswa zilizo kero zetu.

Ni vyema wakajua waziwazi pasipo kuwa na shaka yoyote kuwa rais tunayemhitaji ni huyu:

IMG_20200804_210728_515.jpg

Kwani hayo ndiyo yenye msingi wa majibu kwa kero zetu zote.

Hapendwi mtu hapa!

Kama hayo mtia nia hayawezi ni bora asipoteze muda wake bure. Aende kushughulika na mashamba na mifugo yake. Maana wala hatuta mmiss.
 
Well said mkuu anayepinga hoja zako huyo atakuwa mjinga kama yule mchattle.

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.

Na cha kuongezea ni kuwa mtia nia yeyote ambaye hayupo tayari kutokea kwenye mdahalo na/au kuyatamka yaliyomo kwenye uzi huu bayana, kwa hakika hatufai.
 
Back
Top Bottom