Nafurahiaga saaana jinsi mfumo wa kuishi ulivyotengenezwa na hao waasisi.
Kwamba, kwenye nyumba ya Mwislamu, mkristo anakaa, vivyohivyo Kwa nyumba ya Mkristo anaishi Mwislamu.
Kwamba Paul anaweza kuoa Zuwena na kukawepo Furaha kwenye familia zote mbili.
Kwamba, tunaweza kuanzisha mada ya kuparuana saana, lakini baada ya muda, salamu kama kawaida.
Unaingia Dukani kununua kitu na unapesa yako, ukifika unasema Naomba? Hii ni zaidi ya ustarabu duniani kote huwezi kuikuta hii
Kwamba, Rafiki tu ndio anaweza kuwa wa mhimu kuliko ndugu? Hii iko Tanzania pekee
Kwamba viongozi wa Dini zooote wanaweza kukutana na wakafanya sherehe pamoja, kwamba Sikukuu ya Idd Mkristo anachinja kuku?
Sikukuu za Christmas Mwislamu anasherehekea, Hii haipo kote Duniani
Amani na Idumu Tanzania