edwinito
JF-Expert Member
- Dec 3, 2008
- 210
- 24
Habari zenu wenzangu wote mliosoma Kigurunyembe Sekondari School, Morogoro.
Nina hakika kuna ambao mmeshapata hizi habari za kuwa, baadhi ya wanafunzi waliosoma Kigurunyembe, wako kwenye mchakato wa kuanzisha Kigurunyembe Sekondary School ALUMNI!
Kama huna taarifa hizi, ninachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye Kikao chetu cha 4 kitakachofanyika siku ya Ijumaa, tarehe 24/02/2012, saa 12:30 (Kumi na mbili na nusu) jioni, pale Millenium Tower, Mzalendo Pub!
Nia na lengo la hii Alumni, pamoja na mengine mengi tutakayoyaamua, tumeona ni vema kama siku moja tutakwenda "Shuleni Kwetu" ili kufanya chochote (kupaka rangi jengo/majengo, kuchangia kununua madawati, meza na viti vya waalimu, n.k.).
Pia tunafikiria kufanya misa maalum ya kuwakumbuka walimu, wanafunzi na hasa kumkumbuka mlezi wetu, Father Kanuti (hapa tunawaalika wale wote ambao waliwahi kuishi hosteli pale mchikichini, ingawa walikuwa wakisoma shule nyingine za jirani, mfano: Forest hill, Jabar Hilal, n.k.)
Kama u mmoja wapo, tafadhali tuungane ili tuweze kushirikiana katika kuujenga umoja wetu.
Tunakaribisha pia maoni, ushauri kwa wale walio mbali na TZ.
Mengineyo unaweza kuni-PM.