Kwenye ajira za TRA uwezekano wa Mbara kuajiriwa ni 1 kati ya 100 na Mzanzibari ni 10 kati ya 100, nimekosea hesabu zangu?

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
WAOMBAJI - 135,027

Kwa makadirio kuna wazanzibari 3000, waliobaki wabara 132,027

NAFASI - 1,596

20 % kwa Wazanzibar - 319
80 % kwa Bara - 1,277

CHANCE YA KUPATA KAZI

Wazanzibari - 10 kwa kila waombaji 100 ( 319/3000)
Wabara - 1 kwa kila waombaji 100 (1277/132027*100)
 
Tuna muungano kichomi sana. Na tukiendelea kuuvumilia, utaendelea kutuumiza miaka nenda.
 
Ajira ya mwisho haikuwa hivyo? Why? Application zaidi ya 80% zimetokea bara so aoutomatic wabara wengi ndio hupata nafasi
 
Kama ni wakati wako umefika wakupata hyo kazi hata ikiwa 10/100,000 utapata hyo kazi amini hvyo kuna mtu alifanya interview mpaka za utendaji wa mtaa na alikosa lakini muda wake ulivyofika zilitoka nafasi 5 tena idara kubwa ambayo wengi wanasema hupati bila backup na kaomba nakapata hakuna anaemjua hana mjomba wala shangazi.
 
Wako wengi sana hao watu. People with nothing but mkono wa Mungu. Uko right, muda wako ukifika milango hufunguka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…