Kwenye elimu yetu hapa ndipo Tulipoteleza

MTENDAHAKI

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
4,013
Reaction score
1,447
Watu wanajiuliza sababu za elimu kushuka kiasi cha watoto kumaliza miaka saba ya shule ya msingi pasipo kujua kusoma na kuandika. Hivi kwa wazazi wa leo, tunaokagua madaftari ya watoto wetu (hata wanaosoma English medium) mmeona idadi ya masomo anayosoma mtoto wa darasa la kwanza na la pili.

Naomba niwakumbusha watu tuliosoma miaka ya themanini na mwanzoni mwa tisini. Na leo nagusia madarasa hayo tu kwa watoto wanaosoma English medium.

Kwa mwaka mzima wa darasa la kwanza tulikuwa na masomo 2 yaani Somo la Mwandiko na Hisabati, la ziada lilikuwa ni Kusoma ambalo lilikuwa linatokana na masomo hayo mawili.

Darasa la pili vivyo hivyo tulikuwa na masomo 2 na moja la kusoma. Hakika tulikuwa tunajifunza na tulijua kusoma na kuandika

Hivi sasa mwanangu wa chekechea (Ambako wengine hatukuwahi kubeba daftari kwenda nalo shule wala kurudi nalo) yeye ana madaftari na vitabu 3, kila siku anapewa homework 2

Kila siku kuna meseji anapewa mzazi amsaidie kufanya homework, hivi kama mimi mzazi sijasoma namsaidia vipi,nyie waalimu mna kazi gani

Wa darasa la pili ana daftari saba yaani masomo saba, wa la tatu ana madftari kumi, hivi kweli mtoto mdogo huyu tunategemea asome masomo yote hayo na aelewe?? matokeo ya hakuna kitu mtoto anaambulia,hivyo mzazi kulazimika kutafuta mafunzo ya ziada kwa mwanao.

Nasema tumevuruga elimu yetu sana, ni bora tukarudi kurekebisha tulipoanguka.
 
Kweli kabisa elimu imeshuka vibaya,sisi japokua tulisoma chekechea za kanisa na tulikua tunafundshwa sala sana lakin tulijua kusoma na kuandika kabla ya kuingia la kwanza,sijui ninini kimetokea kwa watoto wetu pamoja na tuition lakini hamna kitu.
 
yaani watoto wanatia huruma, kitoto kidogo begi mzigo limejaa madaftari na vitabu, watawalemaza bure watoto
 
yaani watoto wanatia huruma, kitoto kidogo begi mzigo limejaa madaftari na vitabu, watawalemaza bure watoto

wanafikiri vitabu vingi na begi kubwa ndio elimu bora! Darasa la kwanza anasoma sayansi ya nini hajajua hata kuandika? Pyutuuuuu!
 
kweli kabisa elimu imeshuka vibaya,sisi japokua tulisoma chekechea za kanisa na tulikua tunafundshwa sala sana lakin tulijua kusoma na kuandika kabla ya kuingia la kwanza,sijui ninini kimetokea kwa watoto wetu pamoja na tuition lakini hamna kitu.

Elimu haijaliwi! Ukitembelea vijiji vya tz ndo utajua. Li-nchi likubwa hili halitawaliki wamechemsha kila kitu mmm anzisheni utawala wa majimbo.... Hawataki.kazi kuanzisha wilaya tu na mikoa.wilaya nyingine mpya hata umeme makao makuu (bomani) hakuna! Poor tanzania!
 
wanafikiri vitabu vingi na begi kubwa ndio elimu bora! Darasa la kwanza anasoma sayansi ya nini hajajua hata kuandika? Pyutuuuuu!

watoto darasa la tatu mwandiko mbaya kama kuku anaparaza, sio kosa la mtoto, hakufundiswa mwandiko kama somo, wakati sie darasa la kwanza na la pili ilikuwa ni masomo 2 tu, yaani mwandiko na hesabu (kusoma somo la ziada)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…