Kwenye hospitali ya vichaa, mwandishi wa habari akamuuliza Daktari....

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Kwenye hospitali ya vichaa, mwandishi wa habari akamwuliza daktari:
"Wewe huwa unatambuaje mgonjwa huyu ni wa kulazwa, na huyu si wa kulazwa "?

Daktari akajibu:
"Kuna njia nyingi ... kwa mfano naweza kujaza maji kwenye sinki la bafuni, nikamwekea hapo kijiko cha mezani, kikombe na ndoo;
Kisha nikamwagiza amwage maji yote yaliyo kwenye sinki.

Mwandishi: "Bila shaka aliye timamu atatumia ndoo .. . Maana ndoo ndiyo kubwa! Si ndivyo? "

Daktari: "Hapana! Mtu mwenye akili timamu atafungulia koki ya chini ya sinki!
Tafadhali na wewe nenda kalale kitanda Namba-39 .. . Nitakuja kuendelea kukuchunguza zaidi! "


[emoji3][emoji3] Hah ha haaa!


Hivi kweli na wewe pia uliwaza ndoo?Basi, kitanda chako ni Namba-40 !! [emoji13]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…