Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Wana JF Hii sehemu ya Usajili na usimamizi wa vyama vya siasa kwenye katiba inayopendekezwa baada ya kuisoma nimeipenda.
Sehemu ya 3 ya Katiba inayopendekezwa Ibara ya 224 imeeleza vizuri Usajili wa vyama vya siasa na kuruhusu vyama vya siasa nchini Tanzania kufanya shughuli za siasa endapo vitasajiliwa/chama kusajiliwa kwa mujibu wa sheria.Afu imeweka vizuri kwa kueleza kuwa haitakuwa halali kwa chama cha Siasa kusajiliwa kama katiba yake au sera zake zina mambo yafuatayo;-
1.Kinakusudia kupigania au kukuza maslahi ya imani au kundi lolote la dini,kundi lolote la kikabila, mahali watu watokeapo,rangi au jinsi.
Pia kama kitapigani au kukuza eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano,kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano,Kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa.
Au kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano au hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa kuzingatia jinsi,watu wenye ulemavu na uwakilishi wa pande zotembili za Muungani kwa njia za kidemokrasia.