Kwenye kikosi bora cha dunia hakuna hata mmoja kutoka epl, nini maana yake?

kombaME

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
2,115
Reaction score
2,818
Je ni kwamba hakuna wenye kiwango hicho, au ligi tu mbovu??

Maana duhh mle wamejaa Barcelona tu kama tisa hivi,, epl inatakiwa ijipange kwa kweli... ndo tufunge mdomo sasa, mara sijui hazard, mara aguero, wengine kane, huku wengine sanchez, mara pogba, wengine wakasema countinho.... wote hakuna kitu!!!

Mwaka huu epl tumeumbuka asee.. duuuhhhhh
 
Cha mwakani kipa bora atakuwa david de Gea..wengine sijajua bado.!
 
Kwanza Unabatisha! Wa Barcelona ni Wawili tu! Messi na Iniesta...

Halafu Soka la Uengereza lazima Uliheshimu na Litaendelea Kutoa Ligi Bora Duniani...

Kamata hii! Champion League Uengereza ina Timu 5..

1) Man City
2) Man United
2) Chelsea
4) Spurs
5) Liveepool

Hizi Zote Mpaka Sasa Zinaoongoza Makundi Yao Na Zitamaliza Zikiwa Zinaongoza Makundi...

Hata Huyo Real Aliyetoa Wachezaji 5 anaongozwa na Spurs Katika Kundi Lake...
Halafu Wewe Unaweweseka na Kusema Ligi Mbovu?

Kwanza Ufahamu Kuwa Uengereza Tokea Asili Ligi Yake Haina Sifa Ya Kutoa Wachezaji Bora Duniani! Lakini inazosifa za Kuwa Ligi Bora Duniani...
Na Ndiyomana Timu Zake Hata Zikibeba CL basi Hazitoi Wachezaji Wa Kikosi Bora Duniani...
Only Ronaldo wa Man U did that...
 
Mara mwisho EPL kubeba hilo taji no link?
 
EPL ni ligi pendwa sio ligi Bora hahahaaha si unaona hawapo hapo...angalia wachezaji wa Real Madrid wako watano, Barcelona wawili, Juventus watatu na PSG mmoja... Unaweza ukaona tofauti ya ligi bora na ligi pendwa
 
Iniesta kwa kiwango gani alichoonesha msimu uliopita?


Hapo umetumika Unazi tu! Manake si Yeye, Barcelona wala Spain iliyofanya Cha maana Msimu Uliopita.. Ila Kaingizwa Kwa Sababu ni Barcelona tu isijeonekana ipo nyuma sana dhidi ya Real...
Kwa Hapo Kevin De Bruyne Kwa Midfield Yupo Juu Kuliko Wote hao (Iniesta & Kroos)..
 
wanachoonesha hapo ni LA liga kuwa bora kuliko EPL..waache wahangaike ila ukweli wanao moyoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…