Kwenye maombi na dua zako tafadhali yakumbuke makundi yafuatayo

Kwenye maombi na dua zako tafadhali yakumbuke makundi yafuatayo

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Wakuu najua sisi wote tunapitia changamoto mbalimbali ila tunapofanya maombi na sala zetu naomba tusisahau kuyaombea makundi yafuatayo;

1. Wanawake wote waliobakiza krismasi chache za kusherehekea kabla ya kutimiza umri wa miaka 40 huku wakiwa hawaoni mwelekeo wowote wa kupata mume ambaye watapata nae mtoto.

2. Watu wote walio kwenye madeni yanayowataabisha na kujionasua imekuwa ngumu. Hakika watu hawa wana stress za hatari.

3. Wanaume na wanawake wote wenye wapenzi/wachumba wasio waaminifu ila inaonekana kama kuna nguvu zisizo za kawaida zinazowafanya waendelee kuvumilia upuuzi badala ya kujiondoa kwenye uhusiano.

4. Wanandoa wanaonyanyaswa na wenza wao.

5. Wanafunzi wanye jitihada lakini ikija mitihani huishia kupata alama za chini yaani wanaokesha lakini hawapandishi.

6. Waajiriwa wote ambao kiuhalisia mishahara yao ni ya kuwasaidia kuzuia tu misiba yao ila haiwezi kufanya maendeleo yoyote.

7. Wajasiriamali wanaopambana ila hupata mabalaa kila mara na kuanguka. Yaani hawajawahi anzisha kitu kikaenda vizuri hata miaka miwili.

8. Wazazi wote ambao wametelekezwa na watoto wao. Watoto wanalala five star apartments ila wazazi wanalala kwenye nyumba za mbavu za mbwa. Pia tuwaombee hao watoto wajitambue.

9. Wafuasi wote wa chama cha Mbowe kwa kupotezewa muda wao huku Sultani Mbowe akifakamia asali.

10. Watu wote kama Mdude ambao wanapigania kitu kinachoenda kunufaisha watu wengine na sio wao.
 
Kwa kifupi tuwaombee:
1. Warembo wa zamani waliolinga kuolewa.
2. Wakopaji sugu.
3. Mwanadoa aliyelushwa limbwata.
4. Ndoa zenye migogoro.
5. Wazee wa kukalili/ kumeza point na nukta.
6. Waajiriwa kama walimu.
7. Machuuzi ( tatizo hawa watu ni matapeli fikiria mtu anakuuzia kitu cha 3000 kwa 20000 mabalaa wanayatafuta wenyewe)
8. Wazazi wasiowalea vizur watoto wao.
9. Wanachadema.
10. Wanaharakati.
Tafakuri:
Wewe mtoa mada upo kundi ngani ktk hayo uliyoyasema?
 
Mungu na Baba yetu iliye mbinguni, tunakuomba saidia ulimwengu huu kujua yaliyo mabaya na yaliyo sawa. Toa amani na matumaini kwa wale wanaoteseka kutokana na ukosefu wa haki. Waonyeshe kuwa uko hapo, na unawajali na kwamba utafanya mambo yote kuwa sawa. Mungu, tunaomba ulimwengu uliojaa upendo na huruma..... kwajina la mwanao Yesu kristo.... Amen🙏
 
Back
Top Bottom