Kwenye mazingira gani uliwahi kujikuta umevaa nguo yako nje ndani na ndani nje?

Kwenye mazingira gani uliwahi kujikuta umevaa nguo yako nje ndani na ndani nje?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni mavazi gani hasa umewahi kosea kuyavaa inavyostahili, sio kwa makusudi, ila labda kwasababu ya haraka, kujisahau au giza wakati wa kuvaa, na matokeo yake wakati wa kuvua ndio unagundua ulivaa kinyume na inavyoakiwa...

Au baada ya kufika eneo husika ndio ukastuliwa na ndugu, jamaa au marafiki ulokua nao location, ndio wanakwambia mbona umegeuza vazi lako ndio fashion siku hizi au umekosea? Ndio nawe sasa unagundua umevaa ndivyo sivyo 🐒
 
Nashindwaga kuelewa ndani ni wapi na nje ni wapi kwenye kufunga taulo
😄😄😄😄hasa yale mataulo laini sana huwa haijulikani wapi nje wapi ila haya magumu/mazito yanaoneka
 
Nilikuwa nimelala uchi. Ghafla saa kumi na moja alfajiri napokea simu dala dala yangu imepata ajali na watu wameumia.
Nikaamka nivae niende kwenye tukio.
Nilijikuta nimevaa chupi kichwani! 😀😀😀
 
Nilikuwa nimelala uchi. Ghafla saa kumi na moja alfajiri napokea simu dala dala yangu imepata ajali na watu wameumia.
Nikaamka nivae niende kwenye tukio.
Nilijikuta nimevaa chupi kichwani! 😀😀😀
🤣🤣hii chai mkuu
 
Shikamoo jino 🥶🥶kuna jino lilikua linaniuma mm natupia panadol linapoa maisha yanaendelea kuna siku jioni nimekula nyama nikalichokoza mamaaaaeee nilikua nashangaa machozi yanatoka wakati sijalia nilienda stend saa kumi niwahi gari wakalitoe nafika hosptal yule nesi ananiambia kaka mbona umegeuza tshirt 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom