Kwenye mijadala ya usajili wa wachezaji, Simba wako mtegoni

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kwenye hili suala la usajili wa wachezaji, Simba wameingia mtego wa kifikra na kihisia ambao itakuwa vigumu sana kutoka.

Hakuna timu duniani ambayo wachezaji wote 20+ wa kikosi wana viwango sawa. NASEMA HAKUNA! Wale wa akiba siku zote, ni wa viwango vya chini kidogo. Iko hivyo duniani kote. Hii inazisaidia hata timu kuweza kulipa mishahara wachezaji maana wanatofautiana viwango.

Hata rotations zinapofanyika, huwa ni kwa wachezaji 1-3 at a time kwa wale wa akiba, na kwa hivyo hata mchango wao katika mechi husika unakuwa overall ni chanya. Ndiyo maana nikisikiaga mtu anamnanga mchezaji kama Outtara, huwa nauliza kwa lipi? Nitakuuliza katika mechi 5 zilizopita, performance yake ilikuwaje? Na timu ilipata matokeo gani? Unataka kila beki awe level ya Inonga, timu itaweza kulipa?

Hawa kina Kyombo wamekuwepo hadi timu ya taifa na kwa standard za wachezaji wetu ndiyo wanachukuliwa kama the best. Katika timu ya taifa ukiwatoa hawa wachezaji wa nje kina Msuva na Samatta, unabaki na hawa hawa kina Kyombo.

Wakati mwingine ni wachezaji wenyewe wanakosa spirit ya kujituma na kukuza vipaji vyao. Huyu huyu Kyombo anacheza kwa kuridhika sana, anaona ameshafika. Kuna wakati alikuwa na mwili mzuri wa kimpira, sasa hivi hata muscles miguuni zimepotea. Sidhani kama wa kulaumiwa hapa ni aliyemleta.

Wachezaji wengine wana mchango mkubwa kwenye mazoezi. Hii ndiyo mbinu inayotumia na professional teams. Kuna wachezaji hautawaona katika mechi ila mazoezini wanathaminiwa sana maana wanaweza kuwa pushed kucheza kwa bidii.

Kazi yao kubwa ni kuwafanya wale walio tegemeo wabaki fit na bora. Hapa ndiyo role ya kina Akpan na Kapama inapokuja. Hawa wanatakiwa wajue hawapambanii namba za kina Mzamiru na Kanoute. Ukihukumu viwango vya wachezaji kama hawa unakuwa unakosea sana.
 
Kwa hiyo mashabiki mnapingana na mwekezaji wenu anayehisi kupigwa bilioni yake 1.5 kwenye usajili wa hao wachezaji?
 
Wee nawe sijui umetokea wapi? Tuseme hauoni kuwa Yanga wamefanya usajili mzuri kuliko Simba? Kwamba Singida Big Stars wanaweza kuwa wanaizidi Simba kwa scouting? Watu wengine bhana.😡
 
Kwenye hili suala la usajili wa wachezaji, Simba wameingia mtego wa kifikra na kihisia ambao itakuwa vigumu sana kutoka.

Hakuna timu duniani ambayo wachezaji wote 20+ wa kikosi wana viwango sawa. NASEMA HAKUNA! Wale wa akiba siku zote, ni wa viwango vya chini kidogo. Iko hivyo duniani kote. Hii inazisaidia hata timu kuweza kulipa mishahara wachezaji maana wanatofautiana viwango.

Hata rotations zinapofanyika, huwa ni kwa wachezaji 1-3 at a time kwa wale wa akiba, na kwa hivyo hata mchango wao katika mechi husika unakuwa overall ni chanya. Ndiyo maana nikisikiaga mtu anamnanga mchezaji kama Outtara, huwa nauliza kwa lipi? Nitakuuliza katika mechi 5 zilizopita, performance yake ilikuwaje? Na timu ilipata matokeo gani? Unataka kila beki awe level ya Inonga, timu itaweza kulipa?

Hawa kina Kyombo wamekuwepo hadi timu ya taifa na kwa standard za wachezaji wetu ndiyo wanachukuliwa kama the best. Katika timu ya taifa ukiwatoa hawa wachezaji wa nje kina Msuva na Samatta, unabaki na hawa hawa kina Kyombo.

Wakati mwingine ni wachezaji wenyewe wanakosa spirit ya kujituma na kukuza vipaji vyao. Huyu huyu Kyombo anacheza kwa kuridhika sana, anaona ameshafika. Kuna wakati alikuwa na mwili mzuri wa kimpira, sasa hivi hata muscles miguuni zimepotea. Sidhani kama wa kulaumiwa hapa ni aliyemleta.

Wachezaji wengine wana mchango mkubwa kwenye mazoezi. Hii ndiyo mbinu inayotumia na professional teams. Kuna wachezaji hautawaona katika mechi ila mazoezini wanathaminiwa sana maana wanaweza kuwa pushed kucheza kwa bidii.

Kazi yao kubwa ni kuwafanya wale walio tegemeo wabaki fit na bora. Hapa ndiyo role ya kina Akpan na Kapama inapokuja. Hawa wanatakiwa wajue hawapambanii namba za kina Mzamiru na Kanoute. Ukihukumu viwango vya wachezaji kama hawa unakuwa unakosea sana.
Hivi kwanini Madrid waliitwa The Galacticos??
 
Back
Top Bottom