Kwenye Mkataba wa DP world Watanzania wanapotoshwa!

Kwenye mkataba masilahi ya DP world yako wazi lakini masilahi ya Tanzania yamefichwa( hayajaandikwa).
 
Hawa dp world ni matapeli wataiangamiza Tanganyika

Bahati mbaya mafisadi yamehongwa na waarabu kuwatetea

Watanganyika amkeni
Leta ushahidi kuwa ni matapeli?
kama wapo kwa zaidi ya Nchi 40 duniani zikiwemo za ulaya na hawajatapeli ndio waanze kutapeli Tanzania?
Tatizo watu wanashabikia vitu serious kwa mkumbo kama kushabikia mpira....hata hawatumii akili zao kutafuta ukweli, Shame!
 
Ipo siku mtawaona Dnata nao wanapiga kambi dar airport badala ya Swissport
Dunia inabadilika Yale mambo ya kubebana yanaanza kuisha na ipo siku makampuni yatapewa tenda kwa ufanisi wao na kazi zao bila kuwa na wapambe nyuma wakiwaongezea mikataba kisa wapate percentage

Tunabadilika taratibu ingawa bado sana, yaani siku tukawa na tani 1000 za dhahabu kwenye reserves basi hapo ndio tutajua na wizi umeisha
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Watu mapungufu kibao ulikuwa wapi?
 
Namba 2 Kwa hiyo Sisi tusijali usalama wetu Ila tujali utendaji wao .....tutakuwa hatuna akili
 
Una taaluma ya SHERIA?

Tuanzie hapo.
 
Hujawaelewa wananchi wanataka nini?faida tunaitaka lakini kama mambo yamekaa vibaya kwenye mkataba kama ukomo,uvunjaji haupo hatuwezi kusema tuangalie ufanisi Tu no way Taifa zinapaswa kufaidika na vitu vingiwe viwe na ukomo
 
Kama focus unaandika forcus, utaona mapungufu? Macho huona kile ambacho ubongo hutambua.
 
Mikataba ya TICTS na SWISSPORTS haivunjiki? Haina ukomo? Tukitaka kuendeleza tunawaomba wao? Mikataba hiyo wajibu ni wa serikali ila haki za wawekezaji?

Hizo nchi 40 nao waliingia mikataba yenye vipengele kama hivi?

Watu hawamkatai mwekezaji, wanakataa masharti magumu

Pumbavu
 
Huyu punguani hawezi kukujibu hapa
 
Nikajua kuna jipya kumbe ujinga ule ule tu.
 
Kama walikataliwa Marekani kwa sababu za kiusalama wewe unawakaribisha ?
 
Kumbe ndio maana biashara ya utumwa ilifanikiwa tukauzwa sokoni
 

Kwamba unathubutu kudai Kuwa hujasikia hoja za kiuchumi?

Dk. Slaa: Mkataba wa DP World kama Taifa - Tumeuzwa!

Haina shaka wewe utakuwa kiziwi.
 
Leteni wa kwenu jmn
Hii nchi kweli inamtaka mtu kama Magu mana mkishirikishwa kiongozi haendi mbele

Mlibanwa p.umbu nchi nzima mkawa hamuongei kitu sasa mnajifanya kutaka kumshika kidevu Mama kisa ruksa kuongea
Samia mtakuja mkumbuka sanaa kama Kikwete
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…