Kwenye siasa za Tanzania "Trust No one" ndio kanuni kuu ndio maana Fomu lazima ichapishwe Moja ndani ya CCM

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Mpo salama!

Watu wanalaumu tuu Bure. Oooh! Fomu Moja! Ooh! Sio Demokrasia. Ooh! Kwa nini Sasa!
Kipi hakieleweki?

Mnataka Fomu ziwe nyingi ili katafunua zipigwe sio! Nani ambaye hajui sisi ni Waafrika na tupo Afrika?

Kuchapisha Fomu nyingi kwenye uchaguzi ndani ya chama ni kuonja sumu, kujiwekea bastola mdomoni, kujitia kitanzi. Watu wataanua tanga mapema sana Tena utashangaa wale ambao hukutegemea, Shaaaaa! Watu wamekuweka pembeni unang'aa sharubu.

Hata Mimi nisingekubali

Usiku mwema

Pia soma:
 
Unapochapisha fomu nyingi maana yake umeruhusu wagombea wengine wachukue...
 
Unapochapisha fomu nyingi maana yake umeruhusu wagombea wengine wachukue...

😅😅

Nani atakushauri zichapishwe Fomu nyingi maana kwa akili ya kawaida wewe mwenyewe hutoweza kufikiri kitu kama hicho.

Kwa Afrika endapo utajaribu kufanya hivyo Kuna Asilimia nyingi za kujilaimu baadaye
 
Umenena kweli, watu wanakupigia Makofi huku wanakusagia kunguni ndani ya mioyo yao, hata kama ni wanachama wenzako usijipe asilimia zote, bora fomu 1.
 
Sio kwenye siasa tu. Binadamu sio kiumbe wa kuaminiwa maake time yyt anabadilika
 
Umenena kweli, watu wanakupigia Makofi huku wanakusagia kunguni ndani ya mioyo yao, hata kama ni wanachama wenzako usijipe asilimia zote, bora fomu 1.
Hapo fomu moja na wizi wa kura juu!
 
Lakini kwanini hawamwambii mwenzao ukweli kwamba hatamaliza hadi 2030 ?​
 
Wewe ulitaka zichapishwe ngapi kwani?
 
Siyo kwenye siasa za Tanzania tu bali hata maisha ya kawaida kinachoangaliwa ni maslahi tu.
 
Ni muhimu zaidi kumuamini Mungu pekee, vinginevyo ni ushirikina 🐒
 
Reactions: Ame
Msigwa apewe nafasi ya kugombea
 
Dawa ni moja tu..

Kila anayeutaka u - Rais huko CCM achape fomu yake mwenyewe kivyake, ajaze na siku ya kurudisha wote tukutane pale MAKUTANO JUNCTION mahali zinakopokelewa..

Kama ni katafunua, basi wakatane mitama hapo hapo mpaka kieleweke..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…