Kwenye suala la kuendesha vitega uchumi na rasilimali zetu, Watanzania tuache kujidharau

Kwenye suala la kuendesha vitega uchumi na rasilimali zetu, Watanzania tuache kujidharau

majege

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Posts
237
Reaction score
308
Ndugu zangu nimeona nami nianzishe huu uzi ili tusaidiane kuwaza na kusafiri pamoja.

Hoja yangu inaanzia kwenye hili jambo la Bandari na huu uwekezaji wenye utata.

Mosi: nadhani kama kuna watu wa kubeba lawama ni wale waliyopewa dhamana ya kuongoza serikali kwa kushindwa kusimama kwenye nafasi zao kuwawajibisha wote wanaofanya hujuma zinazopelekea sector zetu za umma kushindwa kuwa na ufanisi na mwisho kukimbilia majibu mepesi ya kuuza ama kubinafsiha tasisi zetu nyeti kama bandari na meeneo mengine ya kimkakati.

Pili: Kumekuwa na teuzi nyingi za kiupendeleo ambazo zinapelekea kushindwa kuchukuliana hatua kali hasa pale ambapo mteule anapopata kashfa za wazi (kushindwa ku-perform).

Tatu: Inaonekana hii nchi sasa hivi inaendeshwa kimtandao zaidi kiasi kwamba watu wakishapangana kwenye timu zao na kuanza kutekeleza agenda zao huwa hawashauliki na hata kupuuza vilio vya wananchi katika jambo husika, ukijiuliza haya yote yanafanyika kwaajili ya faida ya nani? . Kwasababu kama wananchi wanalikataa jambo wewe unayelilazimisha jambo hili unakuwa una-save interest ya nani? Mifano Loliondo, Ngorogoro, Bandari Nk.

Nne: Nchi yetu sasa hivi inawasomi wengi sana tena wa kila fani. Unashangaa wasomi hawa sasa hivi wameingizwa unyonge na wanasiasa kuwa hawana uwezo wa kufanya jambo ukilinganisha na wenzetu wa nchi nyingine na hiki ndicho kinapelekea kujijengea uhalali haramu kwa wenye mamlaka wa kuuza na kubinafsisha kiholela rasilimali za nchi.

Tano: Kwa hili linalondelea sasa hivi kuhusu bandari mimi nashauri kuwa haitakuwa busara tena kufanya biashara na hawa DPW, kwasababu kuna mazingira mengi tata na kwamba iwapo tutayapuuza basi tuwe tayari kuivuna hiyo mbegu tunayopanda leo.

Sita: Nashauri vyombo vya usalama fanyeni kazi yenu mumlinde mama lakini hakikishenii hiyo chain ya majambazi waliojipatchika kwake kama washauri mahsusi inakatwa, vinginevyo hilo joka mkililea litatafuna hadi vizazi vyenu.

Saba: Naomba tukubaliane kwamba mifumo ya kuendesha nchi na pia ushawishi wa viongozi wetu kwa wanaowaongoza naona vime-fail, hivyo nashauri swala la katiba mpya lisipuuzwe kwani litatupelekea kuwa na National concensus, kwasababu kinachotokea sasa hivi viongozi wamerundikiwa powers nyingi alafu wanashindwa kuzi exercise na kupelekea taifa kuangamia.
 
Back
Top Bottom