KERO Kwenye suala ya huduma ya Fibre, TTCL ni wababaishaji sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna namna Shirika haliwatendei haki wateja wake. Kwa mfano, mimi niliomba kuunganishiwa huduma ya TTCL Fiber tangu mwezi wa pili mwaka 2025. Baada ya maombi yangu kupokelewa, nilipigiwa simu na kuambiwa kuwa kungekuja mtu kufanya survey ya eneo langu kabla ya kuunganishiwa huduma.

Hata hivyo, hadi leo tarehe 19 Juni 2026, hakuna mtu yeyote kutoka TTCL aliyewahi kufika kufanya ukaguzi huo wala kunipa taarifa yoyote kuhusu maendeleo ya ombi langu.

Kwa kipindi chote hicho nimekuwa nikijaribu kuwasiliana nao kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, lakini huduma kwa wateja ni duni. Majibu yanachelewa kwa muda mrefu, wakati mwingine hadi miezi inapita bila kujibiwa, na hakuna maelezo yanayotolewa kuhusu sababu ya ucheleweshaji.

Inasikitisha kuona shirika la umma kama TTCL likiwa na mfumo usioridhisha wa huduma kwa wateja, hususan kwenye majukwaa ya kidijitali. Ikiwa shirika limezidiwa na idadi ya wateja kuliko uwezo wake wa kuwahudumia, ni vyema liseme wazi badala ya kuwaacha wateja wakisubiri bila taarifa.

Soma Pia: Huduma ya TTCL Fibre Arusha ni ubabaishaji mtupu, unalipia na kufungiwa hufungiwi huku kifurushi kikiendelea kuisha

Haiwezekani ombi la mteja lidumu kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kutekelezwa wala kutolewa ufafanuzi wa kinachoendelea.

 
Hawataki Hela!
 
Pengine huduma (miundombinu) haijafika mahali ulipo.

Jaribu kampuni zingine.
 
Viongozi wengi wa serikalini walikuwa manyani. Fikiri tu ishu ya maji ya kutumia manyumbani hivi kweli tanzania ni ya kuhangahika na maji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…