Kwenye uchaguzi ndiyo mnao tuangushha

bahatikisiya

Senior Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
139
Reaction score
13
Katika taifa lolote au jamii yoyote kijana ni tegemeo kubwa sana.kijana ndiye mwenye kupanga na kuchagua maisha ayatakayo.kwa namna nyingine kijana ni nguvu ya taifa na jamii.

Lakini badhi ya vijana hawa wamekuwa hawatimzi wajibu wao.hasa linapofika swala la kupiga kura.mara nyingi vijana wamekuwa ni washabiki na wakereketwa wa vyama na viongozi wao bila kuwa wapigaji kura hii ina isikitisha nakukatisha tamaa sana.nimefanya utafiti mdogo ambao siyo rasimi nikagundua kuwa vijana wakikaa vikundi utasikia wakizungumzia chama fulan au mtu fulan lakin ukiwauliza kuhusu kupiga kura kila mmoja atasema la kwake wengi wao walisema hawaja wahi kupiga kura na hawatapiga kura kwa sababu siasa ni mchezo mchafu wengine walisema hawawezi kuendelea kuwapa watu "ULAJI".

Kama vijana tuta waachia wazee wakapige kura na wakati vijana wapo na ni wengi kuliko wazee tuna lipepeleka wapi taifa? Inahitajika elimu ya ziada kuwa komboa vijana hawa wenye mawazo mgando.
 
Usiwalaumu ni mfumo na hali ya maisha ndivyo vinavyowafanya wawe hivyo.
 
siasa zetu zenyewe bado sana hazishawishi watu kupiga kura, zina mandumbwendumbwe mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…