Kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, watendaji na viongozi wa CCM waliwatisha wananchi na kuwabebesha kura feki

Kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, watendaji na viongozi wa CCM waliwatisha wananchi na kuwabebesha kura feki

John Manoni

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2020
Posts
244
Reaction score
167
Wadau,anayedanganya kwamba CCM itaendelea kushinda uchaguzi kwa kura na siyo mtutu wa bunduki ni yule ambaye huwa anasinzia sinzia kama kuku wa kideri,akizinduka hupayuka payuka hivyo.
Kwa uchaguzi wa wenyeviti

Mitaa,vitongoji na vijiji, 2024,kama ambavyo hapakuwa na tofauti na 2019 na 2020,watendaji wa serikali
wanaosimamia uchaguzi pamoja na mapolisi na mamgambo walikuwa upande mmoja na viongozi wa CCM.

Walikusanya watu nyakati za usiku,waliwatisha kwamba atakayetoa habari za wizi wa kura hadharani atafanyiwa kitu kibaya

Usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi wa Novemba 2024,walibebeshwa kura feki za Uenyekiti na ujumbe. Mapolisi na mamgambo walikuwa wanasaidia watu ambao hawakujiandikisha kwenye daftari la mtaa na Kijiji ili wapige kura. Watu walikuwa wanapewa pesa bila kificho ilikushawishiwa,hata walimu walipewa pesa na kutishwa kupoteza ajira.

Mtendaji wa Mtaa wa Nyerere Kata ya Igoma Nyamagana Mwanza alisikika siku ya uchaguzi akisema watu wote wapige kura hata wasiojiandikisha kwani hao wanamsaidia kujaza idadi.

Kwa hali ya uchaguzi hapa nchini ilipofikia, CCM siyo chama kinachoshindana na vyama vya siasa kwenye sanduku la kura. Kulikuwa na uandikishaji wa watoto wa shule kuwa wapiga kura, watoto walishirikishwa uhalifu,ilikuwa hatua mbaya kabisa kwa vizazi vijavyo.

Kwa ujumla, CCM inategemea mapinduzi ya sanduku la kura kwa hongo,vitisho na mitutu ya mapolisi. Ole,kwao waliobatizwa kwa kushiriki na kufurahia yote yaliyoumiza vyama vingine na wanaojua kuwa yule ambaye huwa anasinzia sinzia na akiamka anapayuka ingawa hakuchaguliwa bali alipendekezwa tu,ni mtu mwenye kukosa uchungu kwa wanaodhulumiwa na dola kwa mitutu ya mapolisi kwa sababu yeye amekuwa akilipwa kwa kodi zetu kwa zaidi ya miaka 60+.
 
Ndugu Lissu kwa sasa anasema vizuri zaidi yale aliyowahi kuyasema ndg. Makongoro kumhusu Wasira Masatu. Tangu kwa Nyerere yumoyumo...
Wasira hawezi kupenda uchaguzi wa kidemokrasia,yeye hajachaguliwa,ameteuliwa tu kuwa makamu Mwenyekiti wa CCM.
Hana uwezo wa kutenda miujiza kuondoa ukiritimba wa chama chao.
Nadhani Kikwete angechukua tu huo umakamu,full stop.
 
Demokrasia ya nchi hii haiwezi kuletwa kwa ndoto za watu ambao kazi yao ni kusinzia tu.
 
Back
Top Bottom