ANAUPIGA MWINGI
JF-Expert Member
- Apr 14, 2022
- 389
- 757
Nchi yetu ina pesa yake ambayo ni shilingi ya Tanzania yaani TSH, na hi pesa imegawanyika kwenye kwenye thamani mbalimbali, na hizo thamani ni kama zifuatazo;
50/, 100/
200/, 500/
1,000/, 2,000/
5,000/, 10,000/
Napenda sana kwenye biashara yangu niwe natafuta sarafu za sh 50, 100, 200 na 500 tu, na sitaki kutafuta not kabisa. Wazo langu ni sawa kabisa na wazo la au mfumo wa biashara wa Cocacola na Pepsi, hizi kampuni moja ya sababu ya kuwa na mafanikio ya mauzo Duniani ni kwa sababu wanatafutaga sana sarafu badala ya noti, ukiangalia Tanzania, Cocacola anatafuta sarafu na huwa hatafuti sana not, na hizi sarafu ndio zinazomfanya auze sana soda zake.
Mfanyabiashara kama Bakhresa, ni moja ya wafanya biashara wanaonivutia sana kwenye biashara zao, Bakhresa ukitoa bidhaa zake chache kama Boti, TV labda na Unga, na real estate, bidhaa zake zingine zote huwa anatafuta sarafu, huwa hahangaiki kabisa kutafuta noti na huku kwenye sarafu ndiko pesa nyingi sana zilipo, nina uhakika hata kipindi cha maji ya Viroba Bakhresa alitengeneza pesa nyingi sana kwenye yale maji huenda kuliko bidhaa nyingine yoyote ile.
Kwanini nataka kutafuta sarafu kwenye biashara zangu na sio noti? Najitahidi sana nitafute sarafu kwa sababu zifuatazo;
Sarafu ni pesa ambazo haziumi kabisa, na hii ndiyo siri ya mafanikio ya Cocacola, ndio maana ni vigumu ukutane hata na masikini analalamika kwamba leo amenunua soda, leo kanunua karanga, leo kanunua Ice cream, leo kanunua pipi, leo kanunua andazi au kitumbua au juice, ni vigumu sana kukuta mtu anaumia sana kwa kununua vitu tajwa hapo juu. Lakini leo hii ukinunua hata nguo yash 10,000/ kiasi kuna kuumia kwa mbali na hapa inategemeana na vipato wapo watakaoumia wiki nzima kwa kununu nguo ya sh 10,000/
Sarafu ni pesa ambayo tabaka la chini wanamiliki sana- Tabaka la chini kwa sababu ndio wanunuzi wakubwa pia ndio wamiliki wakubwa sana wa sarafu, hivyo nitakapokuwa na bidhaa za kutaka sarafu basi nitawapata kwa urahisi sana, angali mitaani huko uswazi.
Watu wengi huwa hawapendi kukaa na sarafu mfukoni, watu wengi hupenda kuibadili sarafu na kuwa bidhaa na hapo ndipo watu kama wauza karanga, wauza pipi, wauza, maji, wauza soda wanapopata wateja, wengi wana sababu za kwanini hawapendi kutunza sarafu hasa kutoboa mifuko na au kuharibu vitu kama simu zao na kadhalika, na pia Ombaomba huwa wanafaidi sana hapa kwenye sarafu.
Bidhaa za sarafu, huvutia watu kununua kwa wingi, mtu aweza nunua mandazi 20 kwa sh 2000/
Kwenye ujasiriamali wangu wa kutafuta sarafu, nitajitahidi sana kuzalisha bidhaa ambazo mimi binafisi nitahitaji sarafu, nitahitaji faida za sarafu faida ya Tsh 30, faida ya Tsh 80, faida ya Tsh 15 na kadhalika. Kuwa na bidhaa za kutafuta sarafu zitanisaidia sana kwenye mauzo kwa sababu nitakuwa nimelenga kundi kubwa sana la wale wasio penda kukaa na sarafu, wasio ona uchungu wa kutumia sarafu.
Lakini ili niweze kupata sarafu za kutosha shairiti kwanza nihakikishe bidhaa ninazo zalisha ni zile zinazo weza tumiwa na tabaka zote, Cocacola na Peps moja ya mafanikio yao makuu ni kwamba bidhaa yao ndo bidhaa pekee ambayo ina fiti matajiri na masikini, yaani masikini anakunywa soda na tajiri anakunywa soda, hii ni moja ya mafanikio yao makubwa sana Duniani, na ndo maana wanaweza zalisha au kuuza soda Billion 500 kwa mwaka Dunia nzima.
Ila sasa kwenye Ujasiriamali huu wa kuzalisha bidhaa za kutafuta sarafu huwa kuna siri zake ambazo wengi sana hatuzijui;
Lazima wewe uwe ndiyo mzalishaji na sio muuzaji wa mwisho, kwenye soda wanaopata faida ni kiwanda na sio yule muuzaji wa mwisho, wao wanapata faida kwa sababu ya volume ya bidhaa ni kubwa sana. Ninapopanga na mimi kutafuta sarafu sharti ni hilo hilo kwamba sitarajii kwamba niuze bidhaa za Azam hapana, nikisema niuze bidhaa za Azam, atakayefaidika ni mzalishaji na sio mimi ninayeuza. Viwanda vya pipi mfano, huwa wanapata faida kubwa sana wao kama wao na unaweza kuta kila pipi wanapata faida ya Tsh 5/ sasa kama kwa mwaka wanazalisha na kuuza pipi milioni 1000 maana yake faida yao ni Tsh 1,000,000,000x5=5 Billion hio ndo faida yao wao ya kuuza pipi billion 1 ila kwa muuzaji wa mwisho mwenye duka kamwe huwezi pata hiyo faida kwa kuuza pipi.
Mfano; nikiweza kuzalisha bidhaa yangu na kusambazia wauzaji wa jumla kwa wingi sana nitapata faida kubwa kutokana na volume.
Pia ni lazima Faida yangu mimi kwa kila unit iwe ndogo kuliko faida ya muuzaji wa mwisho, mfano Cocacola tena, unaweza kuta kwenye soda moja kiwanda kinapata faida ya Tsh 50/ ila muuzaji wa mwisho anapata faida ya Tsh 100 hadi 120 kwa kila soda moja anayouza, ila kwa sababu Cocacola wao volume yao ni kubwa basi na faida inakuwa ni kubwa sana ukilinganisha na wauzaji wa reja reja.
Lazima Bidhaa zangu ziweze sana kununuliwa na watu wa tabaka la chini ambao kiuchumi pia wao ndo wanunuzi wakubwa sana, matajiri sio wanunuaji sana wa bidhaa, wanunuaji wengi wa bidhaa ni watu wa tabaka la chini ambao ndo wengi sana na ambao nitawalenga mimi.
Ushauri wangu;
Watu wengi huwa tunakomaa sana kutafuta pesa kubwa ambao mara nyingi sana mtu lazima apige hesabu kali sana kuitoa, lazima ajiulize kuna umuhimu wa kununua hiki kitu au kinawea subiria? Ila sio kwenye bidhaa ya sh 500/ 200/ 100/ au 50/.
Tuwekeze kwenye kuzalisha bidhaa za kutafuta sarafu na sisi tuwe ndo wazalishaji sio wauzaji, ukiwa ni muuzaji kamwe hutaona hiyo faida atakayeona faida ni mzalishaji na sio wewe hapo.
Wengi huwa kweli wanazalishasha bidhaa za kutafuta sarafu kama vile wapika vitumbua, wapika mandazi, watengeneza barafu, watengeneza juice, changamoto kubwa inabakia kwenye volume, wengi wetu unakuta uzalishaji ni mdogo sana ambao hatuwezi iona hiyo faida na pale tutakapowekeza kwenye uzalishaji mwingi basi faida tutaina sana na hicho ndicho Azam anafanya kwenye ice cream zake, juice na kadhalika.
Ujasiriamali wa kutafuta Faida kwenye sarafu ni moja ya biashara nzuri sana na ambayo wajasiriamali hutengeneza Mabilion ya pesa huku sisi tukiona ni kama wanapata faida ndogo sana.

Upvote
13