Theory Au usaili wa Maandishi zingatia sana
1.Dhana ya Udereva ya kujihami na misingi yake mikuu ipo kama 5 hv kama sikosei.
2. Jitahidi Kufahamu Makundi ya alama za barabarani.
3.Magari ya kuyapa kipaumbele uwepo barabarani
4. Taratibu za kufanya pindi unapotaka kulipita au kupitwa na gari lingine.
5. Vitu vya msingi vya kuwa navyo kwenye gari
6.Fahamu Log book na log sheet( Tofauti na matumizi)
7. Wakati wa matumizi ya Taa kubwa
8. Wajibu wako kama.dereva pindi unapopata ajari.
Practical hakikisha vitu vifuatavyo
1.Kufunga Mkanda pindi tu unapopanda gari. Ndiyo liwe zoezi la kwanza kabla ya kuwasha gari
2. Hakikisha unaishika sterling ( Usukani) kwenye mkao wa saa 9 na 15.
3. Kama ni gari kubwa Jitahidi kupanda bila kuudandia au kuji sapoti na sterling.
3.Vaa viatu vya kufunika miguu au sendoz zenye mikanda ya nyuma.
4. Ikiwa watahutaji kukufanyia usaili huku ukirudi nyuma (reverse). Jitahidi kutumia side mirrors Au kale kakioo kadogo kanakokaa pale ndani kwenye kioo kikubwa. Zingatia Usije toa kichwa au shingo nje uchungulie kwa kupitia Dirishani.
5. Jitahidi sana matumizi ya Handbrake,Indicator,Horn
6.Kuendesha gari kwa kufuata taratibu zote vibao na michoro ya alama za barabarani
7. Jiamini tu endesha gari kwa ufasaha bila kuliza gia,Endesha gari kama vile ukiwa peke yako.