Kwenye utambulisho wa Viongozi katika uapisho wa Rais Museveni, Wakuu wa Nchi Wanawake wametambulishwa wa mwisho kabisa

Kwenye utambulisho wa Viongozi katika uapisho wa Rais Museveni, Wakuu wa Nchi Wanawake wametambulishwa wa mwisho kabisa

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
501
Reaction score
1,214
Binafsi leo nimepata fursa ya kufuatilia kwa njia ya television sherehe za uapisho wa Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda huko jijiji Kampala.

Kuna jambo binafsi limeniacha na maswali kadhaa nikijiuliza.

Wakati Rais Museveni anatoa utambulisho kwa wakuu wa nchi (Head of state) walioudhuria sherehe hizo, majina ya wakuu wa nchi wenye jinsia ya kike, walikuwa ndio wa mwisho kabisa kutambulishwa kwenye orodha ya wakuu wa nchi, alianza mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kisha wa mwisho kabisa akawa Rais Sahle Work Zewde wa Ethiopia

Swali ninalojiuliza, je kwenye seniority ya wakuu wa nchi, jinsia huwa ni kigezo kimojawapo au its just concidence tu inetokea majina hayo kuwa mwishoni kwenye orodha ya wakuu wa nchi?
 
Kafuata alphabeti,samia ni s iko mwishoni we vipi?

Kama ni alphabetic order, kwa nini Zimbabwe iwe juu ya United Republic of Tanzania?

Pia kwa nini Ethiopia ndio iwe ya mwisho?

Kwa nini Democratic Republic of Congo ndio iwe ya kwanza?
 
Sijafuatilia inauguration ya Museveni. Hivyo majibu yangu hayako specific kwenye inauguration hii.

Mara nyingi, katika diplomasia za kimataifa, marais waliokuwa madarakani muda mrefu huanza kutambulishwa/ kupewa nafasi kwanza, halafu waliopata urais hivi karibuni hufuatia.

Hii ni kufuata kanuni ya seniority. Waliokaa kwenye urais muda mrefu huanza.

Hivyo, inawezekana wanawake wametambulishwa mwisho kwa sababu wamepata urais mwishoni, si kwa sababu ni wanawake.

In that case, rais wa Tanzania angetakiwa kuwa wa mwisho kutambulishwa, kwa sababu ndiye aliyepata urais mwisho.

Lakini Afrika tuna kanuni kuu ya kutofuata kanuni ingine yoyote pia.
 
Kama ni alphabetic order, kwa nini Zimbabwe iwe juu ya United Republic of Tanzania?

Pia kwa nini Ethiopia ndio iwe ya mwisho?

Kwa nini Democratic Republic of Congo ndio iwe ya kwanza?
... alphabetic order ya jina la mkuu wa nchi sio ya jina la nchi.
 
Obviously hata Mimi ningaanza kuwatambulisha wakiume kwanza,ni dhambi kwenda against nature.
 
Kitu Kama hujui kwanini usiulize? Unaanza kutengeneza shtuma zisizo na msingi?
 
Sijafuatilia inauguration ya Museveni. Hivyo majibu yangu hayako specific kwenye inauguration hii.

Mara nyingi, katika diplomasia za kimataifa, marais waliokuwa madarakani muda mrefu huanza kutambulishwa/ kupewa nafasi kwanza, halafu waliopata urais hivi karibuni hufuatia.

Hii ni kufuata kanuni ya seniority. Waliokaa kwenye urais muda mrefu huanza.

Hivyo, inawezekana wanawake wametambulishwa mwisho kwa sababu wamepata urais mwishoni, si kwa sababu ni wanawake.

Lakini Afrika tuna kanuni kuu ya kutofuata kanuni ingine yoyote pia.

Hiyo hoja ya kuwa madarakani kwa muda mrefu sio kweli, kwa sababu

Kwenye orodho hiyo Rais( mkuu wa nchi) wa kwanza kutambulishwa alikuwa ni Rais Felix Tshisekedi wa Democratic Republic of Congo ambaye ameingia baada ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na baada ya Rais Saliva Kiir wa South Sudan

Pia Rais Samia Suluhu Hassan alimtangulia Rais Sahle Work Zewde wa Ethiopia kwenye orodha hiyo, ambaye ametangulia kuingia madarakani kabla ya mama Samia Suluhu Hassan

Kwa hiyo hoja ya kukaa muda mrefu ni invalid
 
Mkuu, acha kutengeneza maneno...Kama ulimsikia vizuri Museveni na kama ulimfatilia anavyoanza...alisema kabisa "anasoma majina sio kwa Seniority or kitu chochote, anasoma kama yalivyoorodheshwa kwenye orodha na inaweza kuwa labda kwa sababu ya their arrival"

So acha maneno. Lazima ujue chanzo ndo uongee dukuduku lako.
 
Angetambulishwa wa kwanza pia naamini ungeleta uzi.
 
Hapana , kwenye hili kabla ya kuwatambulisha alisema hakuna senior kuzidi wenzake ispokuwa atawatambulisha kwa jinsi walivyowasili(kwa kuwasili kwao kwenye ardhi ya Uganda )
 
Muanzisha mada hajamsikiliza Museveni anavyoanza, au hakumuelewa...kadakia juu juu tu[emoji23]...Halafu amekuja kukimbilia kuanzisha mada[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom