Kwetu mahindi debe ni elfu Tano tu! Huko kwenu hali ya bei ya mazao ikoje?

Hata Sina kinyongo

Senior Member
Joined
May 16, 2020
Posts
118
Reaction score
280
Haijawahi kutokea!

Huku kwetu wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga bei ya mazao hususan mahindi ni yakuridhisha kwa kweli.

Bei ya debe moja kwa mfano la mahindi ni tsh 5000 ilhali kabla ilikuwa ni tsh elfu ishirini!

Kilichobaki ni shukrani zetu kwa Mwenyezi Mungu kwa neema hiyo.

Huko kwenu vipi hali ya mazao?

Mungu ibariki Tanzania na timu ya Yanga.
 
Nyanda za juu debe ni sawa na bure

Rais Magufuli anazidi kuchanja mbunga kutupeleka uchumi wa kati
 
Hapo wakenya wanawatamani kinoma MK254
 
Hapo wakenya wanawatamani kinoma MK254

Huku wapi umeniita, sisi tuna hela za kununua, mlime nyie tule sisi.
Sio lazima kila mtu awe mkulima, Kenya ni kainchi kadogo na zaidi ya nusu yake ni kame tupu, hivyo inabidi tutumie akili kujituma kwa namna nyingine na kununua vyakula.
Nyie huko ndio huwa nawashangaa, pamoja na kuwa na nchi kubwa yenye rotuba na madini na kila kitu lakini bado mnatajwa ndani ya maskini wa kutupwa, LDC.
Nilishangaa kuskia eti sukari imekua tatizo kwenu, uvivu huo.
 
yaani umeandika kwa hisia kali na uchungu moyoni.poleni sana wakenya.
tutawasemee ila msirudie tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyanda za juu debe ni sawa na bure

Rais Magufuli anazidi kuchanja mbunga kutupeleka uchumi wa kati
Mkuu hakika Kichwa chako Ni debe tupu ...yaani mahindi yashuke Bei unasema uchumi unapaa!??tungeruhusiwa kutukana ....!
Hivi unajua asilimia kubwa ya wakulima Tz Ni wa mahindi!
 
Back
Top Bottom