Kwikwi (Hiccups): Chanzo na Tiba (matibabu) yake

al-hamdulillah kwa ushauri wako
 
Ziba pua na mkono alafu vuta hewa ndani kwa mdomo fanya kama alafu meza . Rudia tena haraka haraka bila kuachia hewa itoke nje .jitahidi kurudia kadri ya uwezo wako kwani itakua ngumu kidogo.

Jaribu inaweza kusaidia.

asante mdau,,,ntakua makini na mavyakula ya hamira(nilikula ugali ulochakachuliwa kwa HAMIRA)
 
ikizidi tuwasiliane maana kama kwikwi ya kawaida hamana tatizo lakini kama ile ya kwetu basi tuwasiliane nikupe dawa
 
:a s 465:
Mkuu, una kama siku 5 tangu ulipojiunga jamii forum. Dawa ya kwikwi ni lazima uende hospitali daktari atakuandikia dawa inayofaa kutibu kwikwi, ukiuliza hivyo hapo watu watakuandikia hapa nyingi bila idadi. Kwani nani alikuambia kuwa MAJI NI DAWA YA KWIKWI?
 
:a s 465:

Dawa ya Kwikwi unachukua muhogo mbichi unautwanga au unausaga kwa kutumia blender. Baada ya hapo unaweka maji kidogo ili kupata ile juice then unakunywa kijiko cha chakula asubuhi mchana na jioni. Hakikisha juice inakuwa nzito. Na usistengeneze nyingi kwa sababu huwa inaharibika haraka sana.ukitumia ikibaki unaweka katika friji ili isiharibike. Usitumia juice ulokamua kwa zaidi ya siku moja. Well,utanipa matokeo yake.
 
Mbona kapewa majibu poa tu,mbona humu kuna ma dr.tena specialist
 
Mbona kapewa majibu poa tu,mbona humu kuna ma dr.tena specialist
Hujaelewa nini nimeandika hapa, mpaka sasa hakuna aliyefanikiwa kumjibu kama alivyouliza. Swali lake umemuelewa? specialist ndiyo nani? nitajie specialist mmoja.
 
Hujaelewa nini nimeandika hapa, mpaka sasa hakuna aliyefanikiwa kumjibu kama alivyouliza. Swali lake umemuelewa? specialist ndiyo nani? nitajie specialist mmoja.

We unaona hapo juu wamemjibu nini? au kwako wewe tiba dawa zake ni hospital tu?kuna vitu ambavyo si kila kitu unaweza pata tiba hospital mitishamba na vyakula vingine ni dawa tosha.kuhusu ma specialist kwani hujui watu wanatumia id fake humu?
 
Kwa nijuavyo maji pia hutibu kwikwi hasa ya mda mfupi na isiyo serious.
 
Kwikwi kwa jina la kitalaam inaitwa HICCUP kwa nijuavyo mimi hiyo ni dalili ya kuwepo kwa urea kwenye damu kwa maana ya URAEMIA lakini pia inaweza kusababishwa na irritation of the diaphragm sasa mpaka leo inaaminika dawa ni maji na dexamethasone.
 
Kwa nijuavyo maji pia hutibu kwikwi hasa ya mda mfupi na isiyo serious.
Hata kwa kwikwi serious maji ni ndiyo dawa hasa ya kwikwi. we mara zote ukianza tu kujisikia kwikwi tafuta glasi ya maji, sema inaweza isikusaidie haraka kama unaenda kunywa maji ya baridi sana yale mnayaweka kwenye mafriza na mafriji yenu!. Ukinywa ya kawaida katika joto la kawaida (room temperature), kwikwi haitakawia kuisha.
 
We unaona hapo juu wamemjibu nini? au kwako wewe tiba dawa zake ni hospital tu?kuna vitu ambavyo si kila kitu unaweza pata tiba hospital mitishamba na vyakula vingine ni dawa tosha.kuhusu ma specialist kwani hujui watu wanatumia id fake humu?
Teh! teh! teh!, bado tu ulikuwa hujanielewa?! Si unaona sasa wameanza kumjibu kama swali lake lilivyokuwa linataka. Basi nipotezee chukuwa glasi ya maji unywe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…