Hiyo ya mwanzilishi wa JF na Mtunza Fweza imechomekwa na mwandishi, Israel ni Mwandishi mpambe wa mwakyembe,Watu wa kyela tunajua hivyo..Lakini wapiga kura hawako JF wala majira
Mwandishi ameyajuaje yote hayo? Lazima aliambiwa na mhusika.
Ushauri kwa Bwana Mwakalinga, ametangaza mapema sana kujitosa kwenye kinyang'anyiro na aangalie asije akajikuta anawekwa kwenye kibano cha CCM kwamba alianza kampeni za uteuzi mapema zaidi kabla ya wakati muafaka wa kufanya hivyo. CCM ni chama cha wenyewe na politics za huko ndani wanaziweza wao wenyewe, kwa hiyo inabidi awe makini sana.
Nina hakika ana nia njema sana, lakini watu wasiopenda ushindani wanaweza kutumia nafasi hiyo kumpaka matope. Ile mada iliyofungwa, ilisemekana kwamba yuko Arusha na baadhi ya wana JF wakapaka kwamba ameenda kukutana na "The Big Papaz". Kaa mbali sana hao jamaa (the big papaz) na wala usije ukaonekana unakunywa nao chai hata kama watakuwa wamekualika kwa nia njema, the easiest way ya kukupaka matope itakuwa kwamba umetumwa na hao mafisadi papaz.
Once mtu akipenyeza hiyo agenda ya kutumwa na mafisadi papa, ukizingatia mgogoro uliopo kati ya RA (+EL indirectly) vs Mwakyembe, basi atakuwa amekumaliza kirahisi sana kwa kuwa huo ndio umekuwa wimbo ndani ya CCM na hata kwenye magazeti kwamba wabunge wote walio na ugomvi na RA, jamaa ameandaa watu wake ambao atawa-finance ili waweze kuwashinda wabunge wa sasa kwenye nominations.
Kila la Heri Bwana Mwakalinga, tutaendelea kukumbusha kila tukiona unaenda kinyume na motto ya JF (kumkoma nyani giladi, will you DARE TO TALK OPENLY? - ukitimiza hilo utakuwa balozi mzuri na mwakilishi wa JamiiForum ambayo umeshiriki kuianzisha na kuwa mdhamini wake). Once ukifanikiwa Mbunge usije ukawa kama Dr. Msekela, usikimbie hiki kijiwe, endelea kuja ili tukupe vipande vyako pindi tukiona unachemsha, tukupe ushauri, tukupe maoni na tukukosoe pale tutakapoona umechemka ama chama chako/serikali ya chama chako ikichemsha. Iga mfano wa Bwana Zitto na Mzee wangu Dr. Slaa, hata joto likizidi bado wapo wanakubali kukosolewa na kutetea misimamo yao ambayo wao wanaiamini kwamba wamesimamia upande wa haki.