Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Taifa Ndg. Fadhil Maganya, amedai kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mbeya, inayogharimu zaidi ya bilioni nne iliyojengwa kata ya Busale wilayani Kyela,na kuwataka Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi kujitathmini.
Maganya ameeleza hayo baada ya kutembelea ujenzi wa shule hiyo akiwa siku ya pili ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020-2025, ambapo amesema Serikali imetoa zaidi ya bilioni 4 lakini mradi huo hauonyeshi thamani ya fedha hizo katika utekelezaji.