Elections 2010 Kyela elections!

Status
Not open for further replies.
Hivi huyo JOJI ataendeleza ule mpango wake wakuleta LAPTOP na kuwagawia wanakyela wote kama wapambe wake kina Sikonge, Kanda2 etc mlivyokuwa mnamnadi mwaka jana?
 
Hahahaaaa, yaani sisi na nyie hamna tofauti kabisa. Pamoja na Mwakyembe mwenyewe kukiri kuwa George ni Mkali katika vision ila amwache amalize na Kikwete (sijui ana uhakika gani Kikwete atamaliza mwaka 2015?) lakini nyie bado mnaona kuwa anafaa kwa sababu kawafanya muwe maarufu. Haya bwana, hiyo ni juu yenu. Nilijitahidi niwafunguwe macho ili MFUNULIWE, ila naona ndiyo kwanza blanketi zinazidi.
Mwakalinga hajaanza kusaidia leo Kyela. Kaanza kutoa misaada tangu akiwa Secondary School. Watu wanafahamu hilo na hiyo Kyela FM kwa sasa nusu iko chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyela (Yeye alijitoa. Kama huamini basi nenda halmashauri ya Kyela watakuambia). Ukiona anaandika KBS ujuwe ni yeye ila mengine yote ni kuwa anayafanya kuwa ya Wilaya na yeye anaisaidia tu. Sasa hiyo Redio kafanya kazi zoote na nyie hata kulipa mishahara ya wafanyakazi hamuwezi. Hata huyo Mwakyembe wenu hawezi kusaidia kwa kitu kidogo kama hicho, looo 🙂 Aibu aibu hiyoo. Na huyo ndiyo kipenzi chenu.

Sisi huku Wanyamwezi tunakula tu Hiari ya Moyo wala hatuna hiyana. Ukija wewe kama si wa kuzaliwa pale na huna pesa, itakula kwako kama Mrema. Huku mambo ni kuwa ikifika weekend ni kujirusha kwa taputapu, wanzuki na watoto wanapata Togwa la nguvu huku tukitesa na ngoma zetu za asili: Babu yake Katalambula wa pale Igalula ndiye bingwa hasa maana anaimba kwa mdomo na kupiga gitaa na huku akifunga breki. Na usiku ukifika, kapenzi kanaunguruma hahahahahaa Sikonge raha sana.

YouTube - Nyamwezi-Uwi, mamsanga makumbulage wagela mnyabo


 
NL, heshima ni kitu cha bure. Hizo laputopu si za Kanda2 na zigawiwe Wanakyela? Na ni Kanda2 ndiye aliahidi, sasa nimekuwa mimi?
Hivi huyo JOJI ataendeleza ule mpango wake wakuleta LAPTOP na kuwagawia wanakyela wote kama wapambe wake kina Sikonge, Kanda2 etc mlivyokuwa mnamnadi mwaka jana?
 

kwani kazi ya mbunge ni kutoa Pesa zake mfukoni kusaidia maendeleo, mimi nimefika Kyela mfululizo, kuna misingi ya maendeleo inaonekana.
PITA BARABARA YA kWENDA IPINDA, kumbuka enzi za Mwakipesile, tizama lile Daraja, angalia namna ununuaji wa kokoa ulivyoimarika, vyovyote iwavyo mimi naona kunakitu kimefanyika chini ya mwakyembe kuliko zama za yule Mzee anaelelewa na mafisadi papa .
Mwakalinga aliweka pesa yake katika miradi kadhaa ikiwa ni mtego kwa wana Kyela, wakamng'amua.wakatosa.
Ndugu yangu Mnyamwezi hakuna cha bure, na vya bure aghali, nenda zako Mwakalinga, waliokuzunguka wamekutia doa, umeingia siasa kwa kusukumwa na hao watu wa hovyo hovyo , kizazi cha laana .
 
Asiyekubali kushindwa si mshindani. Get a life dude!
Mkuu, hayo nilishaandika na kutoa PONGEZI kwa Mwakyembe kushinda. Niliandika siku ya kwanza kabisa. Sasa wewe ukirudia tena hayohayo huoni kuwa UNADANDIA train kwenye mbele? Ukifika kwenye sherehe kaa viti vya nyuma ili wakuopoe na wakurushe mbele. Wee unarukia mbele na unakuja kurushwa nyuma, aibu aibu hiyo. Acha kiherehere kama msichana anayebarehe.
lakini Mwakalinga anachangia bila kutegemea kurudisha ? nothing for free, sasa anataka kurudisha tumichango twake, anataka wampe Ubunge.
Mkuu, jamaa kachuma kwa mkono wake bila kuiba hela ya mlipa kodi wa Tanzania. Kama unafikri kugombea ubunge kutamfanya aterereke basi pole sana. Kama aliweza kupata Milioni yake ya kwanza bila kuiba basi nyingine zitakuja pia bila kuiba. najua utakuwa na hamu sana kuona anafilisika. Fisi weee, subiri sana mkono wa binadamu UKATIKE.
 

sioni mantiki yako, katika maneno yako,
Si vibaya kuchangia maendeleo ya kule utokako, si vibaya hasirani.
Kinachokera ni kule kuitumia turufu ya misaada katika miradi aliyowahi kuchangia kama agenda ya kusaidia uteuzi wake katika nafasi hiyo.
mimi nakosoa mtazamo huo, kazi ya Mbunge kwa mujibu wa sheria si kutoa chochote mfukoni mwako kusaidia wapiga kura, nieleze thamani ya Mwakalinga ilipo kama akipata uwakilishi wa UMMA ? kama unahusisha tule tu misaada twake kama sifa ya kuchaguliwa , Je alitutoa aliapate kuchaguliwa ama ?
Umeanza kuishiwa , maana unaanza kutoa lugha za kejeli, hahaaah Great Thinker Sikonge.
 

Umeeleweka Mkuu! Karibu Kyela basi tuchangie mawazo....
 
Hivi huyo JOJI ataendeleza ule mpango wake wakuleta LAPTOP na kuwagawia wanakyela wote kama wapambe wake kina Sikonge, Kanda2 etc mlivyokuwa mnamnadi mwaka jana?

wao wanadai ni sehemu ya maendeleo.
 
Mwanamume wa Makamu huwa na tabia moja muhimu sana ambayo inakutofautisha na mtoto na Mwanamke (samahani akina mama, siyo wote). Wanaume mkiongea jambo moja basi mnamaliza na kuoendelea na mengine. Tabia ya Mwanamume wa makamu kuendelea kulialia kwa jambo lilelile na huku akifahamu ukweli halisi, inanifanya nianze kumchukulia mtu huyo kuwa ana complex moja mbaya sana. Na kibaya zaidi kama anafahamu kuwa anamsingizia mtu asiyehusika kabisa na huo ugomvi.

Mambo ya kutumia mafumbo kusema watu hapa, nimeyavumilia na kukaa kimya kwa muda mrefu sana. Si kuwa siwezi kuongea ila hiyo siyo kawaida yangu. Ila hata Chatu ukimbana sana mwisho wake huwa anang'ata. Naanza kuona mwisho wangu utakavyokuwa maana yakiendela basi sintakuwa na jinsi zaidi ya kuanza kujibu mapigo na mwisho nile KIFUNGO CHA IP milele. Max Mello, anza kujiandaa kunifungia.

Mlio na ugomvi wa moja kwa moja na Mwakalinga basi MSUBIRINI arudi hapa. Msinihusishe kwenye GOMVI zenu na Mwakalinga. Mnikome kama mlivyokoma ziwa la mama zenu. Kama hili halikuhusu basi usijibu maana utakuwa IDIOT.
 
Ujumbe umekufikia. Fisi asubiri tu mkono wa mtu ukatike. Wengine usiwasubiri chini, wafuate juu......
 
Ujumbe umekufikia. Fisi asubiri tu mkono wa mtu ukatike. Wengine usiwasubiri chini, wafuate juu......

hahaaaah , Mwakyembe atakua Mbunge wa Kyela hata Roho ya majungu ikikuuma kwa jina la unafiki, pole mkuu.
labda afe, akiwa hai, atashinda kama unabisha endelea na matanga ya Mwakalinga maana hata fufuka tena, Mwakyembe kwako ni Jinamizi baya, jina lake likitajwa unazimia roho.
 
Sawa Mkuu, umeshinda maana sasa naona umeanza utoto.
 

ize ize ize ize Sikonge,

Usifikie huko mkuu, kwenye ushindani kuna kushinda na kushindwa. Sehemu pia ya ushindi ni kwa washindi kushangilia ushindi na washindwi (hivi hiki ni kiswahili kweli?) kulia kwa uchungu (kumbuka mechi ya Ghana v's Uruguay?).

Take it easy..... kuna watu hapa wanafurahi sana kuona ukiumia zaidi (hata mimi nilikuwa mmoja wao kwa siku mbili zilizopita ila malaika wa MUNGU amenishukia na kuniomba niwe mpole).

Kumbuka pia kuna watu walichukizwa sana na tambo za timu Mwakalinga hapa JF. Kuna watu walichukizwa sana na matusi ya timu Mwakalinga hapa. Hii kwa sasa ni pay back time mkuu. Elewa tu kuwa kushangilia ushindi ni part ya mashindano.

Usifikie kwenye kujishusha chini kiasi hicho.

Sasa ukiondoka, nani ataongoza kampeni ya Dr Slaa hapa? think about that for a moment
 
I am no longer convinced that Mwakyembe is as clean as he would want us to beleive. Haniingi akilini jinsi gani mwanasheria aliyebobea anayeshindwa ku-declare conflict of interest wakati anshikilia nafasi nyeti na kubeba jukummu zito la kitaifa. Nadhani wanaJF wanakumbuka sakata la kampuni yake ya energy, wakati akiwa m'kiti wa kamati ya Bunge for the same. Kwa kweli niekuwa na moyo mzito tangu nigundue ukweli wa jambo hili. Ninampongeza kwa kushinda, na kuwashinda wale waliyotaka kumnyima haki yake...lakini ninakaa chonjo nikisubiria siku Mwakyembe wa kweli anajitokeza. And I would be pleasantly suprised if that doesn't happen. But until them machale yananicheza na kuniambia WATCH THIS SPACE!!!
 

Bange tu hizi
 
.

Ndiyo, ushindi wake umenifurahisha sana,Lakini baado ninawasiwasi na kuondolewa jina lake.Kumbuka kuwa kyela kulitokea kashfa za kadi feki zaidi ya 10,000 na nasikia mbunge zilimlenga moja kwa moja. Na taarifa zemepelekwa wilaya,mkoa na kitaifa.

Masanilo kweli wewe inakuingia akilini kwamba jimbo la kyela linawanachama wa ccm zaidi ya 20,000 na waliopiga kura za maoni ni 20,000.wewe ni mwalimu sijui hapo kama hakuna combinations za figure.

Hapa kwetu mwanza(Nyakato -Buzuruga) ni salama kabisa.Tumechagua mbunge wetu kwa hali mpya na moyo mmoja.
 

http://bible.gospelcom.net/bible?passage=Luke+23:26&language=english&version=NLTInanikumbusha biblia kuna yule jamaa anaitwa Simon wa Kirene, alimua kubeba msalaba wa yesu!Mat 27:32 na Luke 23: 26 Imekuwaje nawe umeamua kuwa vuvuzela? Umetumwa?
 
Mwafrika,

Mna kila haki ya kushangilia ushindi wa Mwakyembe. Mie hilo wala sina HASIRA nalo. Nilichoandika ni kitu kingine kabisa tofauti na UCHAGUZI. Ingelikuwa uchaguzi basi ningelikuwa mie ndiyo naleta UTOTO.

Kweny uchaguzi, Washenzi nyie Mwakyembe timu (maneno ya AS hahahaaaaa 🙂 mna kila haki ya kurusha makombora. Niliongea na AS akasema "........*nina zao was***** wale saa hizi wananisubiri nije JF wanitukane, hahahaaha, sijihuko sasa hivi........"

Gia mliotumia kushinda ni kubwa sana. Yaani kura 17,000???? Mhhh Nyie wakali. Naona Kyela inaongoza kwa kuwa na CCM wengi kuzidi hata Dar es Salaam. Nina imani hata wewe moyoni unafahamu kabisa KALUFUNDI Kamechezwa.

Hapa nipo nimejichimbia saafi kabisa nikijiandaa kuanza kampeni kwa ajili ya Dr. Slaa. Akitangaza kipenga basi nitaenda ARDHINI. Uchaguzi haufanyiki JF mkuu. Malecela alisema "ushindi unapatikana ardhini" na siyo angani au kwenye MITANDAO. Hivyo, nikifungiwa kwa kumwaga mboga, haitakuwa hasara sana. Kifungo hicho ntakiomba mwenyewe kabisa. IP BAN FOR LIFE.
 
nakubaliana nawe , uko sahihi . WAKATI WAKUFURAHI NA KUFURAHI, wakati wakugonga glass na kusubiri NEC ya CCM tuone itaingia kwene mtego wa kina Lowassa na Mafisadi papa nchini.
Mwakyembe kila la heri kuelekea uchaguzi mkuu, ingawa siipendi CCM, lakini utumishi wake kwa umma wa Kyela kama mwakilishi wao Bungeni umenifanya niamini wewe ni tegemeo kubwa kwao, kundi la Mwakalinga liendelee na kulialia , mkisubiri Huruma.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…