Kyiv -Ukraine sasa hali tete.

Kyiv -Ukraine sasa hali tete.

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeonya kuwa Urusi inaweza kuzidisha mashambulizi dhidi ya miundombinu ya kiraia na vituo vya Serikali katika siku zijazo

Matukio makubwa kaka mji mkuu wa Kyiv yamepigwa marufuku hadi Alhamisi, kabla ya Siku ya Uhuru wa Ukraine kesho, kufuatia onyo la mashambulizi ya Urusi kwenye mji huo.

Amri iliyoongezwa ya kutotoka nje pia imetangazwa katika mji wa kaskazini-mashariki wa Kharkiv na itadumu hadi Alhamisi

Inafuatia onyo kutoka kwa Rais Volodymyr Zelensky Jumapili kwamba Urusi inaweza kujaribu kitu kibaya wakati wa kuadhimisha kumbukumbu hiyo, ambayo inajiri miezi sita baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

Wakati huo huo, Rais wa Urusi Vladimir Putin ametaja mauaji ya Darya Dugina, binti wa mmoja wa wafuasi wakuu wa Urusi kuwa ni uhalifu mbaya.

Hapo jana, Moscow ililaumu idara za usalama za Ukraine kwa shambulio la bomu lililomuua msichana huyo mwenye umri wa miaka 29.

Kyiv imekanusha kuhusika.
1661254981803.gif
 
Back
Top Bottom