Kylian Mbappe na safari ya Barack Obama kutoka magheto ya Chicago

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
.
"My story is the part of the large American story" Namkumbuka sana MwanaAfrika Mashariki, mtoto wa Mzee Hussein Obama akisimama nyuma ya Microphones pale Chicago akihutubia wapiga kura, namkumbuka Barrack Obama kwenye mbio zake za Urais
.
Obama aliweka wazi kwa kujiamini kuwa stori yake ni sehemu ya stori ya taifa kubwa la Marekani, kilichotokea alitwaa Urais wa taifa hilo kubwa, ni miaka imepita macho yangu yanadondokea kwa mtoto kutoka mitaa ya Bondy Ufaransa, asili yake Cameroon na Liberia, Kylian Mbappe
.
Mbappe ana mtihani kama wa Obama jioni ile ya 2008 pale Chicago, safari ya mtoto huyu ilianzia pale visiwani Monaco kwenye dimba la Stade Louis, aliwastua Wafaransa, alibisha hodi kwenye lango kubwa la historia ya soka lao
.
Nachotaka kuwaambia ni kuwa taifa lile halina tabia ya kuwapamba sana watu waliofanya makubwa kwenye soka lao, sahau kuhusu Raymond Kopa, Thierry Henry na Michel Platin, hawa wote licha ya ubora wao hakuna hata mmoja aliyepewa heshma ya sanamu (statue) watu mioyo yao ya baridi tu
.
Sanamu pekee ni la Zinadine Zidane, ilimchukua muda msanifu Abdel Abssemed kuliandaa, lakini sio kwamba ni sanamu la kumsifu mtoto wa mitaa ya La Castallane, Marseille bali ni sanamu la kuwakumbusha vizazi kuwa Zidane alifanya ujinga kumpiga Matterazzi kichwa, tukakosa kombe kwa ujinga wake
.
Nageuka kuitazama miguu ya Mbappe, najaribu kuwaza atabadili upepo huu?? Ataweza kujengewa sanamu bora kukumbusha vizazi juu ya ubora wake??, Nafikiria mchezaji wa kwanza kinda kufikisha mabao 15 UEFA, nafikiria ni mchezaji wa kwanza wa akiba kupiga hatrick UEFA
.
Nafunua tena ukurasa nagundua licha ya miaka yake 21 ni mchezaji ghali namba mbili duniani, naendelea kufahamu kuwa ni kinda wa pili baada ya Pele kuingia kambani kwenye fainali za kombe la dunia, bado nawaza alikuwepo sehemu ya kikosi cha mastaa ila alidhihirisha ubora wake
.
Bado nawaza mabao yake 90 kwenye mechi 120 za PSG na assists 49 naona kuna kitu, naiona tena historia ya Mwafrika kwenye historia ya taifa kubwa kama Ufaransa, akifika miaka 28 naamini sanamu litakuwepo pale Paris! Tuombe uzima
 
Ni kama heshima yake itatunzwa,tatizo lipo hapo katika kukubali michango ya watu wengine hasa katika michezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…