Msaada unahitajika wa jinsi ya kumwokoa huyu mwl wa taaluma mwenye tabia ya kuwataka kimapenzi wanafunzi wa kike ktk sekondari hii. Nikiwa mwl wa nidhamu nilimwita faragha na kumwonya kwa kumweleza madhara na athari ya tabia yake hiyo. Alitulia kidogo tu, hakubadilika bali kabadili tu mbinu. Anajihami kwa kulaumu kuwa watoto wa kike hawana nidhamu/heshima. Huwatongoza na wanapokataa yeye huwachapa viboko na kuwatishia adhabu mbalimbali. Je ungekuwa ktk nafasi yangu na una nia ya kuwaokoa wanafunzi hawa bila kumwangamiza mwalimu wewe ungefanya nini?