La huyu mwalimu na wanafunzi wake wa kike kisheria inakuwaje?

KEFODAW

Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
34
Reaction score
2
Msaada unahitajika wa jinsi ya kumwokoa huyu mwl wa taaluma mwenye tabia ya kuwataka kimapenzi wanafunzi wa kike ktk sekondari hii. Nikiwa mwl wa nidhamu nilimwita faragha na kumwonya kwa kumweleza madhara na athari ya tabia yake hiyo. Alitulia kidogo tu, hakubadilika bali kabadili tu mbinu. Anajihami kwa kulaumu kuwa watoto wa kike hawana nidhamu/heshima. Huwatongoza na wanapokataa yeye huwachapa viboko na kuwatishia adhabu mbalimbali. Je ungekuwa ktk nafasi yangu na una nia ya kuwaokoa wanafunzi hawa bila kumwangamiza mwalimu wewe ungefanya nini?
 

  • Kwanza waweza kuwatumia walimu wenzake wa kiume ili wamuelimishe kwamba anachofanya hakistahili kabisa, kama hajabadilika.
  • Mshirikishe hili swala mkuu wa shule. Ili amwite na ampe onyo na aelezwe wazi kama hatojirekebisha basi swala lake litafikishwa kwa mkurugenzi kwa hatua zaidi za kisheri.
  • Ni kosa kwa mwalimu kutembea na mwanafunzi,akibainika na sheria ikichukua mkondo wake atakuwa hana ajira na miaka 30 jela inamsubiri.
 

Unaulizia njia ya kwenda peponi bila kumuacha shetani? Endelea kuulizia labda dr ngwadodo kutoka tanga atakuja na jibu
 
wewe una matatizo
si mfukuzeni tu?
au mhamishieni shule ya wavulana,high school...
 
Na huu ni ushahidi mwingine wa kutokuruhusu viboko shuleni!Kwani wataonewa sana watoto wetu wa kike kwa kisingizio eti hawana adabu kumbe wanatishwa watoe ngono.Nakushauri usimfumbie macho wala kumlinda huyu mharibifu!Kama umemuonya na hataki kuacha,mwekee mtego na kisha achukuliwe hatua kali!Hakuna sababu yoyote ya kumlea.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Asante sana mkuu kwa ushauri. naahidi ntaufanyia kazi.
 
Lol...nakushukuru sana Vocabulary!, Ama kweli kwa vile nahitaji kuiona pepo, sina budi kumtosa moja kwa moja shetwani. thanx alot for your advice!
 
Shukrani sana Mwl.RCT; kwa ushauri mzuri. I promise to work on it and give u the feedback.
 
hapo unatakiwa kuwaokoa hao wanafunzi kwa kureport issue kwa polisi ili akamatwe kwa ubakaji (kutembea na msichana chini ya miaka 18 ambaye si mkeo) bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…