Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Miamba ya soka nchini Hispania,Ulaya na Dunia kwa upande wa klabu, FC Barcelona na Real Madrid jana walishindwa kutamba mbele ya wapinzani wao baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1. Barcelona walilazimishwa sare ya idadi hiyo ya mabao na Atletico Madrid uwanjani Camp Nou.
Barcelona waliongoza kupitia Rakitic (dk 41) lakini Atletico Madrid walisawazisha kupitia Angel Corea (61) aliyefunga bao hilo kwa mpira wake wa kwanza kuugusa tangu aingie uwanjani humo. Barcelona walimaliza mchezo huo bila ya Messi (dk 59) na Busquets (dk 51) ambao walibadilishwa kutokana na kuumia.
Nao Real Madrid walilazimishwa sare nyumbani Santiago Bernabeu na Villarreal. Bruno Soriano alitangulia kuwapa bao Villarreal (dk 45) kabla ya Sergio Ramos kusawazisha katika dk ya 48. Real Madrid inaongoza La Liga kwa alama 13 ikifuatiwa na Sevilla yenye alama 11 na Barcelona yenye alama 10 katika michezo 5.