La mgambo limelia jamani natangaza sensa ya wanaume wasiopenda mawigi!

Mheshimiwa amefata ushauri wa JF. Kuna siku nilisoma wanasema nywele ziko ovyo. Mnaona! Mtu akiwa natural mnachonga, akiweka dawa mnachonga. Huyu mama niliona picha yake juzi juzi, humu humu watu wanasema mbona nywele hazieleweki. Sasa hapo mnasemaje wadau?
 
Aisee naomba niwe wa kwanza kwenye hiyo sensa, napinga miwigi ya aina yoote na minywele artificial! Hiyo midude inaniput off ile mbaya! Yaani utakuta inachomachoma hivi! huwa nahisi kila kitu feki!
 
Natamani niombe picha za wasichana wenu nione, sio mnatuzuga hapa. Si hajabu hilo wigi ndilo lilikufanya umtokee.

Aisee naomba niwe wa kwanza kwenye hiyo sensa, napinga miwigi ya aina yoote na minywele artificial! Hiyo midude inaniput off ile mbaya! Yaani utakuta inachomachoma hivi! huwa nahisi kila kitu feki!
 
Sijui nisemaje.... mawigi yananiboa sana. Nywele za bandia? Tena unakuta mwanamke kajichubua halafu kaweka wigi na lipstiki nyeupe kama unga, makucha marefu na rangi kwenye eyelids za juu, ana pengo na kajipulizia marashi ya ajabu ajabu. Haya, inasemwa kila mtu ana haki ya kuwa atakavyo. Sina tatizo na hilo lakini wigi linakera sana. Sana.
 
...achilia wigi, hata anayesukia rasta, sijui human hair bla blah, wote wananikera!
pheeww,...

acha niendelee kushabikia wenye Orijino singa na kipilipili kama cha Lizzy!
 
Haaa. Kazi mnayo. Mimi wangu tena kama sijasukia weaving muda mrefu ndio kwanza ananikumbusha. Kwa hiyo msi generalize.
 
Reactions: Mbu
Haaa. Kazi mnayo. Mimi wangu tena kama sijasukia weaving muda mrefu ndio kwanza ananikumbusha. Kwa hiyo msi generalize.

LOL, anakukumbusha? ana hila huyo! ha ha ha (am joking!)
kisa cha kuyachukia hayo 'manyangarika' kichwani ni;
  • siku mrembo anapokwenda kusukia hizo weaving, atachukua si chini ya masaa sita! what a waste!
  • wengi wanaovaa mawigi, time ya kulala wanayavua na kubakia na mabutu mabayaaaa kichwani!
  • wengi wanaosukia rasta, siku mbili tatu za mwanzo hawataki uwachezee nywele, eti unawaumiza!
  • binafsi napenda mlimbwende aliye free kushikwa/kuchezewa nywele, hata ikibidi ku shower pamoja.
(I hope watoto wamelala saa hii, hawasomi jf)
 
Natamani niombe picha za wasichana wenu nione, sio mnatuzuga hapa. Si hajabu hilo wigi ndilo lilikufanya umtokee.
Wanawake wa kiafrika mwapendeza sana na nywele zenu za kawaida, zinahamasisha kweli. Mi wangu ni dread locks kwenda mbele kitu, kitu nechero!
 
Mbu hapo umeng'ata patamu!
 
Reactions: Mbu

Bahati mbaya sioni pakukong'oli 'thanks'. Ningekong'oli mara 2.
 
Aisee, unatumia soda gani? Ebu agiza waambie bili kwangu.
 
wakati kuna wengine wanaona dreadz ni uhuni! kila mtu na preference yake bana.japo nywele articial kero yake ni kunuka jasho,coz the head never breath! kuna siku mtu aliniomba nim'style nywele,kidogo ninge-puke!nikajiuliza pillow yake huyu inabidi mume aiweke alama manake ukiilalia utaota uko jehanam! afu unakuta mtu kaweka mi-human hair ya blonde,anakuwa kama chizi! hivi na wanawake hawahesabiwi wasiopenda hii mikitu?
Wanawake wa kiafrika mwapendeza sana na nywele zenu za kawaida, zinahamasisha kweli. Mi wangu ni dread locks kwenda mbele kitu, kitu nechero!
</p>
 
Nasubiri michango mingine zaidi ili nihitimishe hii mada. Bahati nzuri michango inajibainisha waziwazi kuwa imetoka kwa mtu wa jinsia gani. La mgambo limepulizwa kualika wanaume na siyo wanawake. Pamoja na hayo, bado nitatambua michango ya akina dada kwa namna ya kipekee zaidi. Karibuni wadau hususan wanaume kuchangia mada. Nachotaka kujua ni je, wewe binafsi unapenda mkeo au girl friend wako avae wigi? Wanaume wengine wamefika mbali zaidi wanapochangia hoja hii kiasi cha kutaka kupre-empty nilichoanza kuhitimisha lakini bado mawazo ya wanaume wengine ni muhimu kuongeza uzito wa hitimisho.
 
...achilia wigi, hata anayesukia rasta, sijui human hair bla blah, wote wananikera!
pheeww,...

acha niendelee kushabikia wenye orijino singa na kipilipili kama cha lizzy!

mh,kazi ipo leo.
 
Wanawake wa kiafrika mwapendeza sana na nywele zenu za kawaida, zinahamasisha kweli. Mi wangu ni dread locks kwenda mbele kitu, kitu nechero!

Keep it up; namshukuru aliyeanzisha thread hii! Itasaidia sana kina dada wengi!
 
Yaani nachukia mawigi mno, inabidi tupange siku kila mwanamke anayevaa anavuliwa hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…