Laana ya Bella Gutman na mateso ya Benifica

FananiMedia

Member
Joined
Jul 29, 2021
Posts
28
Reaction score
87
Tenda wema nenda zako,usingoje shukrani.

Ukingoja shukrani utakuja chelewa, Huu ni msemo wa wahenga pia ni sehemu ya mstari wa wimbo wa bendi ya msondo ngoma...

Ni msema maarufu sana ambao uko dhahiri kwenye maisha ya kila leo.

Miaka ya 60 wakati mataifa mengi ya Barani Africa yaki ng'ang'ana kudai uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa kizungu barani ulaya vita ya soka ilikua ndio inapamba moto.

Hii ni baada ya kuanzishwa kwa michuano ya Klabu bingwa ulaya mwaka 1956 na kwa miaka mitano bingwa wa ulaya alikuwa mmoja tu Real Madrid.

Baada ya fainalo 3 za kubeba kombe Waliingia fainali mwaka 1960 wakakutana na Benfica ya Ureno ikiongozwa na kocha Bella Gutman raia wa Hungary mwenye asili ya kiyahudi.

safu ya ushambuliaji alikuwepo mtoto wa kimakonde toka Msumbiji kwa kina Luis Miqquisone bwana Eusebo.

Real Madrid waliishia kufungwa siku hiyo Benfica walitawazwa mabingwa wapya wa Ulaya huku vijana hao wa ureno wakipiga soka Biriani siku hiyo

lililowaacha watu vinywa wazi kwa kutoka nyuma kwa goli mbili na kumaliza kwa kushinda 5-3.

Mwaka mmoja baadae Benfica waliingia tena fainali na Barcelona na wakashinda tena wakatawazwa kuwa mabingwa wa Ulaya kwa miaka miwili mfululizo.

Ulaya ikashangazwa Dunia ikashangazwa Mashabiki wa Benfica wakajihisi wanaiona pepo katika ardhi ya ureno.

Mara baada ya fainali ile dhidi ya Barcelona Kocha Gutman aliwafuata viongozi wa Benfica na kuwaomba wamuongezee mshahara

Viongozi walikataa Baada ya majadiliano ya muda mrefu huku viongozi wakikataa kata kata kuongeza mshahara,,Gutman aliondoka.

Lakini hakuondoka hivi hivi Aliwaambia Viongozi ya kwamba haitakaa itokee ndani ya miaka mia moja Benfica kutwaa ubingwa wa Ulaya Akimaanisha kwamba Benfica haitatwaa Ubingwa wa Ulaya ndani ya miaka mia moja Viongozi wakachukulia kawaida Alipoondoka ni kama aliondoka na ufunguo wa mafanikio ya Benfica ulaya.

Miaka michache baadae wakaingia fainali ya ulaya wakapoteza ikachukuliwa kimichezo Tangu siku hiyo mpaka sasa Benfica wameingia fainali nane za Ulaya na wamepoteza zote Nane.

Inasemekana laana ya Gutmann inawaandama Kupoteza fainali nane sio kitu cha kawaida Haijalishi wapinzani wana ubora kiasi gani...

Kuna wakati wali ingia fainali ya Ulaya na staa wao Eusebio akaaenda kutembelea kaburi la kocha wake Gutmann kuomba msamaha lakini haikusaidia kitu usiku wa fainali kipigo kilisimama pale pale.

Fainali ya karibuni ni fainali ya Europa mwaka 2013 dhidi ya Chelsea na waliishia kufungwa 2-1

Mwanzo ilichukuliwa kama masikhara lakini sasa imekuwa hivyo pengine laana ya Gutman bado itawatesa zaidi benifica miaka 57 bila ubigwa wa ulaya na kupoteza fainal 8 inafanya watu waamini kua laana hiyo ipo!

Miaka ya karibuni viongozi wa Benifica walijaribu kufika katika kaburi la Bella Gutman pale Budapest Hungary alipozikiwa kuomba radhi ila bado laana iko pale pale...

wamekuwa wakitawala ubigwa wa ndani ila linapokuja suala la ubigwa wa ulaya wamekuwa wanafeli Mara zote

pengine mwaka 2063 yaani miaka 42 ijayo ili itimie 100 toka laana ya gutman benifica watakuwa mabigwa .
 
Very interesting...
 
Hii laana ya Bella Gutman mtu ataona uzi huu kama kichekesho ila Benfica amepoteza sana fainali.Yeye alisema miaka 100 Benfica hawatachukua kombe la club bingwa ulaya.na miaka 50 hakuna club yoyote ya ureno itatwaa kombe lolote la ubingwa wa ulaya mara mbili mfululizo.Na wenyewe au mchezaji unakuwa ushaathirika kisaikolojia tena ukienda kuchezea Benfica ukifika fainali wazo la laana ya Gutman linatawala mwisho ndiyo vile mnaikosa fainali.mfano mechi ya fainali na Sevilla dah.au fainali na Chelsea.zoote walipoteza.Mzee enzi hizo alikuwa kocha kweli alishinda kila kombe linalotakiwa kushindwa na timu.kiujumla yeye alichokitaka ni sawa na mtu kama Ferguson wa Manchester united.Au Wenger na Arsenal watu kama wale walikaaa Club muda mrefu na makombe mengi walishinda lazima hata wakiondoka waondoke vizuri na siyo kwa ubaya.Gutman alikuwa sahihi kwa upande wake na hakuwa sahihi kwa upande wa wengine laana aliyowaachia Benfica.Huwezi kumfananisha Gutman na Haji Manara hata kidogo.Manara alikuwa msemaji tu.kwa wale ambao hawamjui Gutman labda waende Wikipedia historia ya club alizofundisha na timu ya taifa pia ameshinda makombe.
 
Balaa balaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…