The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
LAANA YA FAMILIA.
Karibu binti na mwana wa Mama Afrika.
Mtu au Familia Fulani zina laana au mikosi fulani ambayo, ukiifuatilia unaweza gundua ni jambo la kurithi au la kizazi na kizazi.
Pengine linaweza kuonekana ni jambo la kawaida sababu huwa lazima limkute au limtokee yeyote au mtu fulani katika familia au ukoo.
Iwe magonjwa fulani ya ajabu, vifo, matukio ya aina fulani, kupata hasara, kuunguliwa, mikosi, bahati mbaya nk.
Kuna familia au mtu akifikisha umri fulani, anapata ugonjwa fulani, Kichaa nk.
Kila anayeinuliwa kielimu, ajira, akifikia hali fulani anapoteza maisha, ajira au kuna jambo fulani baya hutokea.
Laana huleta chuki, uhasama, mauaji, uchawi na gomvi za ukoo au familia moja na nyingine.
Hayo hutokea pale ambapo familia fulani hufanikiwa au kuwa duni kiuchumi kiasi familia nyingine kuhisi, wale ndiyo chanzo cha sisi kuwa hivi, hasa imani za kishirikina.
Mambo ya kishirikina yapo, lakini si sababu kubwa ya kufanya laana fulani kutawala Familia za wengi.
Sababu kubwa ni laana za kifamilia au ukoo.
Kuna watu wana macho, midomo, tabia zinazoweza kuendana na uchawi au ushirikina lakini kiharisia hayo mambo hawayajui kabisa.
Maneno, kauli, matendo, hisia huumba.
Kabla sijaja na somo la nini tunafanana na Mungu, nitangulize nguvu za uumbaji katika vinywa vya watu.
Kuna mtu akikasirika na kusema jambo baya dhidi yako linatokea. Kuna mtu anaweza kusema neno lolote kimzaha kisha linatokea.
Mbali na wanaosemea wengine, kuna wanaojitabilia wenyewe na yanatokea. Kujibashiria si lazima iwe kwa maneno au kwa mawazo.
Mawazo, maneno huumbwa na hisia. Hisia au maneno, ndiyo mlango mkuu unaoumba maisha yetu( nitachanganua hili katika somo lijalo, usiyejuwa, utajua sala ina mahusiano gani na hisia zako ) .
Kwa wenye laana fulani za kifamilia, wengi hukimbilia kwa Waganga, ambako huchochea moto zaidi kwa kuongeza laana juu ya laana.
Mfano.
Babu wa babu yako aliuwa mtu na kabla yule aliyeuawa ajafa, alimpa laana babu ya babu yako.
Laana ile ikaanza na babu yako, ambaye alianza kuanguka kifafa akiwa na miaka kumi na nane.
Kisha mtoto wa babu yako ambaye ni baba yako akapatwa na kifafa akiwa na miaka kumi na nane, na kisha kati ya wanao kuna mtu anaanza kuanguka kifafa katika umri kama huo.
Ukiamua kutafuta ufumbuzi hata ukaenda kwa mganga au katika maombi, huwezi kutatua tatizo.
Sababu mzizi ni haki ya mtu ambayo haijalipwa.
Na kama utapata mkosi ukaenda kwa mganga na hisia za kuhisi mtu fulani.
Hisia zako zitamsaidia mganga kumdhuru huyo mtu ambaye hana hatia.
Na yeye sababu ya uchungu wa madhara ya ulichomfanyia anaweza kutoa laana nyingine ambayo italeta madhara hata katika kizazi chako kijacho.
Kizazi chako nacho kikifanya kama wewe, kitajikuta kikiandamwa na laana nyingi mno na hata kusababisha uwe ni ukoo Wenye kuandamwa na madeni ya laana.
Laana zipo zenye kutokana na mikasa mbalimbali.
Kubwa ni mauaji, dhuruma za mali, mapenzi, kupuuzia haki ya mtu, na Kufunua siri zenye laana.
Mauaji si lazima ya mtu tu, hata kuuwa viumbe wengine bila sababu. Viumbe kama paka, mbwa, ng'ombe, kuku, bata, n.K.
Viumbe wana mambo mengi tofauti na watu tunavyowachukulia. Kila kiumbe kina nguvu Katika eneo fulani.
Mfano paka anaweza asitumike katika tiba, lakini ana nguvu ya kubeba vitu.
Mbuzi anaweza asitumike kubeba vitu, lakini ana nguvu katika kafara. Kwa hivo kila kiumbe kina nguvu eneo fulani sababu ni roho kama wewe, tofauti wewe una mamlaka ya kuvitawala.
Katika eneo hili laana nyingi upatikana hasa kwa kuua kimakusudi kiumbe na uzao wake. Au kudhuru wanyama usiojua ni wa nani. Mfano unaua mbwa na watoto wake, Au kiumbe fulani chenye mimba.
Dhuruma za mali hii inajulikana, lakini dhuruma za Mapenzi kidogo ina utata.
Sababu hapa kuna laana nyingi mno.
Kama unajua umeingia katika mahusiano ya kimapenzi na mtu ambaye hutoweza kumuoa au kuolewa naye, bora usimsumbue na kumuacha na kinyongo.
Kuna watu vinyongo vyao havipiti bure, na wengine hawakubali yaishe, wanazunguka kudai haki zao.
Bora wanaodai haki zao Madhara unaweza ukayabeba mwenyewe.
Lakini hawa wanaokufa na vinyongo wakati mwingine madhara unaweza usiyaone kwako.
Watoto au kizazi chako ndiyo wanaoweza kubeba.
Mfano , leo mwana umechezea binti wa mtu, na kumuacha isivyo haki.
Wewe unaweza baki salama, mabinti zako wakaja kulipia ulichofanya leo na hata kuwa ni kawaida.
Unazalisha binti wa watu, kisha unamtelekeza yeye na mwanaye, unadhani ukikwepa laana ya maneno ya mama utakwepa na laana ya lawama za mtoto?.
Kupuuzia haki ya mtu.
Wewe ni shahidi, lakini kwa sababu binafsi unatoa ushahidi unaopelekea madhara makubwa katika maisha ya asiye na hatia, mbali na kupoteza maisha unakuwa ni kati ya waliosababisha mateso kwa mtu.
Laana yake utaibeba tu, kama si wewe basi kizazi chako.
Kufunua siri zenye laana.
Kuna watu wanasafisha laana na kuzitupia katika viumbe wengine au kuzirudisha kwa wahusika.
Unaweza kuona kiumbe au mtu kichaa, ukabaka, ukaua usijue ndiyo umechukua ile nafasi ya deni au kilichotupiwa.
TUWE PAMOJA.