Laana ya kichwa cha wendawazimu yahamia kwa dada zetu

Laana ya kichwa cha wendawazimu yahamia kwa dada zetu

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Tanzania ilikua imelitawala soka la kike la Afrika Mashariki kwa zaidi ya miaka 10 au zaidi. Kwa kifupi tulikua hatuna mpinzani si Kenya wala Uganda. Lakini miaka ya hivi karibuni wenzetu wameonekana kuamka na kuanza kufanya vizuri wakati sisi tukiendelea kuishi kwa historia.

Mwaka jana Kenya wamechukuwa ndoo pale Azam Complex huku timu yetu ikizidiwa kila kitu na kuchapwa 2:0. Baada ya hapo kuna mashindano yalifanyika Uganda ya u17 timu yetu ikatoka matuputu, nazani Uganda walikua mabingwa. Wengi walisema ni bahati mbaya.

Jana kwenye mechi ya kufuzu kombe la Dunia chini ya miaka 17 kwa wanawake timu yetu imeondolewa kwa aibu baada ya kupigwa Hamsa 5:0 na Uganda.

Haya ni matokeo mabaya kabisa kwa timu yetu ya wanawake kwa miaka ya karibuni.
Inauma na kusikitisha kwani timu za wanawake ndio ilikua tegemeo pekee la kutufikisha kwa haraka World Cup siku moja.

Nilichokibaini ni dada zetu kulewa sifa, uteuzi wa timu mbovu usiozingatia ubora wa wenzetu hasa katika nguvu, vipaji na maumbile, Timu kucheza aina moja ya mchezo mwanzo mwisho na TFF kumpa majukumu mengi kocha Shime.

Wamempa timu takribani 4 peke ake. Mi naona Shime anaelemewa na hivyo kushindwa kupata muda kuwasoma vijana wake vizuri akiathirika na ule msemo wa mshika mawili.

Kenya na Uganda tayari wameonesha dalili ya kutupita. Sio muda Burundi na Rwanda watatuacha. Kwa matokeo ya jana TFF wajitathimini kama wanataka soka la kike litukwamue. La sivyo naiona ile laana ya kichwa cha mwendawazimu ikihamia kwa dada zetu.

Tatizo tuna kawaida ya kuridhika na mafanikio madogo madogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba ndio wameanza kututia nuksi ya kufungwa goli 5 , wameambukiza dada zao
 
Hizi timu za Wanawake mbona zinafanya vizuri mara nyingi tu. Au unasubiri wateleze ndio uje kuanzisha uzi?!
 
Back
Top Bottom