dygie
New Member
- May 31, 2023
- 2
- 1
“Labda kesho nitafanikiwa…Labda ni kwa kua sikusoma...au Labda sina nyota”. Ni msururu wa mawazo unaopita kwenye akili ya kijana Rakimu ila siku asubuhi kabla ya kuamka na kufungua dirisha na kugundua kuwa kila kitu kipo kama alivyokiacha jana.
Jiji kubwa na tupu la Dar-es-Salaam linamtazama usoni kwa hasira kali sana, lisimwonee hata chembe ya huruma Rakimu. “Nani alaumiwe kwa ugumu wa maisha ninaoupata?” Kila siku Rakimu anajiuliza tena na tena.
Rakimu anaamka kila siku na kufungua fremu yake ndogo ndani ya soko changamfu la Kariakoo, madeni ya kodi, ushuru mkubwa na mambo mengine kibao yanamwandama kijana Rakimu kama yanavyowaandama vijana wengine wengi katika nchi tukufu ya Tanzania. Kila kijana anaamini kuwa atafanikiwa lakini wengi wanaendelea kusota kwenye wimbi kubwa la umasikini.
Wafanyabiashara kama akina Rakimu wamekua wakipiga kelele kuhusu maumivu yanayokumba biashara zao kwa ajili ya ushuru na kodi, yani mtu mwenye kibanda cha mtumba tu anapaswa kulipa ushuru kama mtu mwenye kiwanda. Swali lililo kwenye vichwa vya vijana hawa ni moja tu “Je, ni haki?”.
ya swali kama hili ni mengi sana midomoni mwa watu, kwa sababu kila mmoja anajua japo moja au mawili kuhusu elimu ya Uraia, shukrani ziende kwa mfumo wa elimu unaopigiwa kelele za kila namna katika nchi hii.
Ahadi zinazoweka mwanga ndani ya roho za wapambanaji katika kujenga Taifa bora ni nyingi mno, hata baadhi ya waliozisikia wakaanza kuhoji uhalisia wa ahadi zile.
Rakimu akiwa katika shughuli yake kwa bahati akapita mwandishi wa chombo kikubwa cha habari. Na bahati ilikua kwamba yule mwandishi aitaka kusikia maoni ya wazi ya Rakimu juu ya Ubora na Uwajibikaji wa uongozi uliokuwepo madarakani.
Rakimu alishusha pumzi ndefu sana, baada ya sekunde kadhaa akaanza kusema kwa utulivu mkubwa “Ndugu mwandishi nina mengi ya kukwambia”.
Mwandishi akamwambia “Nina shauku kubwa ya kuyasikia”, basi Rakimu akatizama kibanda chake na kisha akamtazama mwandishi akasema “Nilishawishiwa sana kupiga kura kwenye uchaguzi uliopita…Sikuwa naona maana ya kushiriki uchaguzi kwa kuwa haujawahi kuniletea mabadiliko nnayoweza kukumbuka”.
Mwandishi akatikisa kichwa kuonesha kuelewa hisia za Rakimu, Rakimu akaendelea kusema “Nikasikiliza propaganda za wanasiasa wengi sana, na kwa bahati niliowakubali ndio waliopita. Kwa sasa ni viongozi wangu na wawakilishi wangu huko serikalini.
Sitaki kukosa shukrani kwa kusema hawajatimiza chochote walichosema, lakini? Kwa nini masuala makubwa sana kama ushuru ninaotozwa sijawahi kuona yakirekebishwa? Kiukweli ndugu mwandishi ningependa viongozi wetu waone sababu ya kuwajibika ili kutimiza ahadi zao, tunaumia wananchi”.
Mwandishi akamshukuru sana Rakimu kwa mchango huo na akajazia kuwa vyombo vya habari ndo mahala haswa pa wakereketwa kupazia sauti zao. Basi yule mwandishi aliandaa makala safi na baadae jioni, Rakimu akasikia sauti yake redioni.
Pamoja nayo, maelezo yakinifu ya kiongozi wa taasisi husika yakatolewa. Swali jingine likaja kichwani kwa Rakimu “Je shida ni uongozi? Au ni uwajibikaji wa viongozi?”. Swali hili ndo lilimvuruga kabisa kijana Rakimu akaamua kula Ugali wake na maziwa ya mtindi illi apumzike tena akiamini kuwa Kesho itakua bora kuliko leo.
Basi zoezi la kula lilimalizika na akajitupa kwenye kitanda chake ambacho anashindwa hata kukumbuka alikitandika lini, akatazama dari la chumba chake. Maswali mengi yakazidi kupita moja baada ya jingine, na mara nyingine maswali yalishindwa hata kufuata foleni yakagongana hovyo na kusababisha msongo wa mawazo kwa Rakimu.
Katikati ya vuguvugu hili baadhi ya mambo yalikua yaijirudia kwa sauti za juu sana kwenye kichwa cha Rakimu kama vile “Kwani nani anapaswa arekebishe sharia za ushuru?” na “Hivi itachukua muda mrefu kiasi gani, na garama kiasi gani kurekebisha hizo taratibu?”. Suala ambalo lilijionesha wazi kichwani kwa Rakimu ni kwamba Sio ngumu sana kufanya marekebisho, Inawezekana kabisa.
Muafaka huu ukazua tena swali jingine “Kwa nini mambo hayabadiliki?”. Mara ghafla Rakimu akaanza kukumbuka foleni kubwa ya magari iliyosababisha daladala aliyokuwa amepanda ichukue Zaidi ya saa mbili kufika kwenye kituo alichokizoea kabisa cha takriban mwendo wa dakika ishirini.
Kabla wazo hili halijapotea gafla redio ya umeme aliyokua anasikiliza nayo ikazima gafla, Rakimu alikasirika sana akajiuliza “Serikali yetu ina tatizo gani?
Asubuhi tu ya siku hiyo rafiki yake Rakimu alikua analalamika akidai kuwa ili mambo yabadilike lazima uongozi ubadilike, basi Rakimu akaendelea kumsisitiza kua mabadiliko ya viongozi sio ya lazima tatizo kubwa ni uwajibikaji wa viongozi waliopo.
Walibishana sana kwa muda mrefu bila kupata jibu muafaka ambalo kila mmoja wao anaona linafaa. Katikati ya dimbwi la mawazo hayo Rakimu akapitiwa na usingizi tena. Wazo la mwisho akilini kwake likawa labda kesho itakua bora Zaidi.
Ni kweli kwamba vijana wengi wanapambana ila kiukweli kitu kinachotakiwa haswa kubadilishwa ni namna ambavyo jasho la watu hawa linavyowafaidisha wao wenyewe.
Serikali ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia matunda ya kazi za mikono ya wananchi wake inapaswa kuchukua hatua na kuwajibika kwa manufaa ya wote.

Upvote
3