SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Niliwahi kutoa ushauri kwa Yanga kujikita kwenye kombe la shirikisho maana wameonyesha wana uwezo wa kukomaa na kuchungulia ubingwa kabisa. Baada ya ushauri ule nilishambuliwa sana na mashabiki lia lila wa Deportivo de Utopolo.
Leo nawageuzia kibao wana Lunyasi wenzangu. Simba imeonyesha kupata ugumu kupata tiba ya kuvuka hatua ya robo fainali na msimu huu imevuka hatua ya makundi kwa kutumia nguvu sana maana karata zake za kwanza haikuzicheza vizuri.
Hivi ikitokea Simba akaangukia Shirikisho CAFCL kwa makusudi au kwa bahati mbaya (tukichukulia kwamba CAF haitayafuta haya mashindano), kwa kikosi hiki hiki cha kina Jobe na mbinu za ndani na nje ya Uwanja ambazo imeweza kujifunza kwa miaka hii 5 iliyopita, naona uwezekano wa Simba kufanya vizuri sana. Pia itasukumwa na matokeo ya Yanga ya msimu uliopita ya kufika fainali kwa hiyo lengo halitakuwa tena nusu fainali bali fainali au kuchukua kombe kabisa.
Sasa hivi utani wa jadi kati ya Simba na Yanga umebadilika kabisa. Sasa hivi ni mbio za nani atakuwa wa kwanza kubeba kombe la Africa, na labda atakuwa wa kwanza kwenda kwenye Kombe la Dunia la Vilabu.
Sioni Simba ikienda kurekebisha makosa na mapungufu yake kwa hiyo ikirudi CAFCL tusitegemee maajabu yoyote yale. Nasema hivyo kwa sababu dalili zimeanza kuonekana. Viongozi wa Simba na mashabiki wake wamepigwa na upofu au maslahi binafsi na siyo mapenzi kwa timu yametuvuruga wote.
Yanga ikiongeza mtu kama 2 hivi za maana na kupata kipa bora #2, mwakani inaweza kufika mbali zaidi ya mwaka huu kwenye CAFCL.
Pitia pia uzi huu:
Ushauri: Yanga ijikite Kombe la Shirikisho