Labda United tunasubiri hadi malaika aje aseme kwa niaba yetu

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
Yupo binadamu aliwahi kusema ukweli ni dawa kwa aliye tayari kuupokea. Mwingine akasema kama unacho cha kusema na kisha ukachagua kukaa kimya, hiyo ni tafsiri nyingine ya uongo.

Ni nani mwenye ujasiri wa kuuzungumza na kuusikiliza ukweli Duniani? Pale Manchester United upo ukweli unaombagua mnenaji.

Ilianza kwenye kinywa cha mwendawazimu Jose Mourinho, bila kupepesa macho aliiambia Dunia pamoja na mataji mengi aliyowahi kuyabeba, kumaliza nafasi ya pili akiwa kocha wa Man united, yalikuwa ni mafanikio makubwa katika kazi yake.

Tulimsikiliza kama tumsikilizavyo H baba, kisha tukaendelea na mambo yetu. Angel Dimaria mmoja wa mawinga bora kabisa wa kizazi hiki alikuja na madai kuwa Man United walimsajili kwaajili ya kuuza jezi tu. Naye tukampa kipande kilekile cha sikio, tusikilizacho stori za Lukamba na wake zake hivi sasa.

Akaibuka Alexis Sanchez ule usajili uliokuja na mbwembwe za kupiga piano siku ya utambulisho wake, akatabiriwa makubwa, nyuma ya jezi yake namba 7, unajua kilichomtokea?

Anasema siku ya kwanza anakanyaga Carrington, uwanja wa mazoezi wa Man united, alimuomba wakala wake amrudishe Arsenal. Yeye tukamsikiliza kama kero ya kengele iliyotukuta tumeshaamka tayari. Tukampuuza vilevile.

Raph Ragnik yule Director wa Michezo aliyepata bahati ya kuwa bosi wa Man Unite bila kutarajia, wakati anaondoka alishauri timu ifumuliwee muundo mzima. Kuna mengi sana nyuma ya kamera inayokuonesha Pogba na Lingard wakishangilia kwa kucheza pale Fly Emirates.

Zlatan Ibrahimovic hakuzungumza kwaajili ya kuchekesha pale aliposema kuwa akiwa Man United ilimbidi apunguze Euro milion 1 kwenye mshahara wake kwaajili ya kujinunulia matunda.

Kama mtu hajali kuhusu mahitaji yako, kwanini wewe ulijali jasho lako kwaniaba yake? Yuko wapi Mkhitaryan na kipaji chake?

Tujiulize inakuaje timu ya Sir Alex Ferguson ambayo kiungo alikuwa Tom Cleverley ilibeba mataji alafu timu yenye Bruno Fernandez inahangaika hata kuingia nne bora?

Kwanini vipaji vingi vinapotua Man United vinashindwa kutenda kama vilipotoka? Huyu ndiye Anthony tuliyesimuliwa balaa lake? Kama ni mchezaji mbovu kwanini Man United walilipa pound milioni 80 kwa Harry Maguire?

Nilishangazwa sana pale niliposoma mahali, eti sababu moja wapo ya Man United kumsajili Delay Blind, ilikuwa ni yeye kumiliki wafuasi wengi Instagram. Kisha mshangao wangu ukapata majibu pale Louis Van Gaal alipotoboa siri kuwa Man United ni timu ya kibiashara.

Baada ya wengi kulia na kupuuzwa, mshindi mara 5 wa Balloon D or, kasema na Dunia imemakikinika upya kabisa.

Cr7 ambaye anazijua lugha nne, yaani Kireno, ki Italiano, Kihispania na Kingereza, yeye kachagua kuzungumza ukweli. Kwa bahati mbaya kauzungumza nyakati ambazo ubaya ulishamtangulia.

Mashabiki walishamuona akigomea sub, wakamuona akiondoka kabla ya mechi kuisha, upo mchoro uliokwishakamilika kwenye vichwa vyao kuwa yeye ni mbaya kwa taswira ya klabu.

Sasa utawaaminisha kipi tofauti? Ikiwa namba zimeshamkataa mtoa hoja, Man United bila Ronaldo wameshinda mechi asilimia 70, Man United wakianza na Ronaldo wameshinda asilimia 25 pekee. Baada ya kuambiwa ukweli, wao wakachagua kumchukia aliyeuleta. Ni ajabu.

Ni hawahawa mashabiki waliokuwa wakipiga makelele na mabango ya "Glazzer out", leo katokea jasiri wa kunena hadharani kuwa Glazzer ni tatizo, wamemkasirikia mnenaji.

Ukweli una marafiki wachache sana, na uongo utabaki kuwa uongo hata uaminiwe na Dunia nzima.

Umefika wakati wa Man United kushughulika na hoja na siyo mtoa hoja, itafutwe sababu kwanini imekuwa timu kubwa isiyoogopwa tena.

Wasimsubiri malaika aseme kwaniaba yao.

 
[emoji28][emoji28][emoji28]

Nakuelewa mkuu. Ronaldo kuuponda uongozi wa Man U kwa sasa, ni kama Bashiru kuiponda serikali. Watu wanaruka na yeye, na sio hoja zake!

Ila kuna hatua fulani ukifika, inakua ngumu kusikilizwa hoja zako. Hata kama ni hoja zenye mashiko.

Anyway, Mwanitesa United mnahitaji mabadiliko makubwa kuanzia kwa wamiliki, uongozi, benchi la ufundi, mpaka wachezaji!

Bila hivyo, mtapata tabu sana!
 
Kabisa mkuu inatakiwa reform ya hali ya juu sana
 
Uzuri Cr7 number zake zinaongea kwa vitendo. Ana magoli mengi kuliko watu wote kwenye michuano rasmi.

Hivyo kwa mtu anayeelewa mambo hauwezi sema Cr7 ni mbovu kwa sasa wakati miezi michache iliyopita alikuwa kwenye tatu bora ya kuwania kiatu cha ufungaji bora wa Epl msimu uliopita.

Binafsi pale Man U kuna shida kubwa ngazi za juu yaani wamiliki na viongozi waandamizi ndio maana kila mchezaji akifika kiwango chake kinapwaya.
 
Basi Kuna uchawi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…