Ladha ipi ya juisi huwezi kuichoka?

Ladha ipi ya juisi huwezi kuichoka?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Habari wana jukwaa,

Kama mada inavyojieleza. Ni ipi ladha ya juisi huwezi kuichoka hata unywe mara nyingi.

Kwa upande wangu mchanganyiko wa nanasi, parachichi na pasheni. Kwa kweli napenda sana mchanganyiko huu na ile harufu ya pasheni ndio naburidika kabisa.

Hii hata uandaaji wake sio mgumu, chukua nanasi menya, kata vipande vidogo menya parachichi kata pia vipande na pasheni kisha weka maji kidogo kwenye brenda na yale matunda kisha saga.

Baada ya hapo chuja waweza weka sukari kidogo kama ni mpenzi wa sukari nyingi maana nanasi lina sukari.

Enjoy.

1617802661280.png
 
Ukwaju mixer passion kwa kusindikiza chips. Miwa kwa uchovu
 
Sema kweli juisi ya limao siwezi sahau. Kwanza raisi sana kuanda na ni chach mpka rahaa. Ukinywa mara moja unajikuta tena unataka na ukiwa una mumunya mdomoni unasikia raha.
Nzuri ukiweka na kachumvi kadogo.

Ni nzuri mana ni chanzo kizuri cha vitamini C na pia inazaibia kuamsha vimeng'enya chakula.
 
Juice ya pera ndo tamu sijawai ona.
 
Back
Top Bottom