Habari zenu wakuu,Hongereni naona weekend ishaanza kukolea,mi nilikuwa naomba kuuliza hv ladha ya kupigwa BAN ikoje???maana kuna siku nilivamia Uzi mmoja hv ilikuwa ni alfajiri sana nikakuta mdau mmoja anatukana sio pole pole yaani alikuwa anajaza thread page peke yake lakini yote aliyokuwa anaandika yalikuwa matusi tupu ila kikubwa nilichokiona alikuwa anaomba kupigwa BAN sasa muda ulipofika kweli akapigwa BAN.Sasa nimebaki najiuliza hv BAN tamu???,mtu akipigwa BANanafungiwa wapi maana yule mdau sijamuona kitambo kidogo humu natamani nikamtembelee huko SELO nimuulize ladha yake.Mwenye ulishawahi kuonja ladha yake msaada wa maelezo kidogo.