Hili jambo mbona huwa nalisema mara nyingi. Majina ya jinsia zote yanajirudia kwenye nyadhifa fulani.
Ni vigumu ukutane na DJ anaitwa Richard au Benjamin, kama ana hilo jina mchunguze nyumbani au mtaani atakuwa na jina linalotumika sana zaidi ya hilo. Na bado atakuwa na a.k.a yake ya kazi
Vigumu kukutana na CEO wa benki mbongo anaitwa Frank, Jerome au Abuu, utakutana na Benjamin, Mohammed au Hussein. Kwa wanawake utawapata kina Nancy, Lorraine na Miriam kwenye urembo na umiss na waolewe na wachezaji au mastaa. Kina Zuena, Maria, Asha, Janeth huwa hawaolewi na waenda gym kujaza misuli. Vigumu usikie first lady Afrika hapa anaitwa Marylin.
Kuna majina nikiyasikia huwa nayakataa kwa kazi fulani. Benjamin Mwakyembe akiomba kuwa DJ namkatalia. Ila Alexander Tozi akiniomba kuwa accountant nakataa. Huwa natamka jina mfululizo najaribu kuliita na kulinganisha position, lisipokujakuja trust me halifai hiyo nafasi. Huwezi kuwa na Rais anaitwa Kelvin Melkisedeki