Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Getty ImagesCopyright: Getty ImagesLady Gaga ametangaza donge nono kiasi cha dola za Marekani 500,000 kwa yeyote atakayewarejesha mbwa wake wawili baada ya mtu mmoja kuwaiba na kumpiga risasi mtu aliyekuwa akiwatembeza mbwa wake.
Tukio hilo limetokea siku ya Jumatano majira ya jioni huko Hollywood, kwa mujibu wa vyanzo viwili vya mwanamuziki huyo.
Vyanzo hivyo vimesema mwanamuziki huyo wa miondoko ya pop anatoa kitita hicho cha nusu milioni kwa yeyote aliye na mbwa wake, na awasiliane kwa barua pepe KojiandGustav@gmail.com kujipatia zawadi hiyo.
Majina ya mbwa hao ni Koji na Gustav.
Aliyekuwa anawatembeza mbwa hao alifikishwa katika kituo cha afya cha to Cedars-Sinai, na hali yake ni nzuri, kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na Gaga.