manchoso
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 1,605
- 2,055
Haijalishi mmekosana nini ni wakati sasa kukaa mezani musameheane haya maisha tu afu ukizingatia mshakuwa watu wazima
Tumefundishwa kuwa binadamu hatokuja kupenda kamwe hadi pale atakapompenda anaemkuchukia.na mukumbuke kuwa msamaha ni kitu tunachokitoa kuwapa wengine ila kiukweli ni zawadi tunayojipa sisi wenyewe.
Na unaposamehe haimaanishi unalazimishwa kusahau kuna ubaya m
wingine hausahauliki lakini haupaswi kumchukia mtu bali unapaswa kuchukia matendo yake.
Wakati mwingine Mungu huzungumza nasi kwa matendo hivyo labda misiba hii imetokea labda iwe sababu ya Judith kumaliza ugomvi wako na clouds kwani tunafahamu ndio iliokulea na tulianza kukufamu kupitia tasnia ya sanaa ukiwa mtangazaji na mwanafamilia wa clouds siku zote tumetamani sana kuona ugomvi wenu unakwisha .
Kuishi kwa amani na mapenzi ni muhimu sana hasa kwa nyakati hizi, dunia leo imekuwa sio tena sehemu salama ya kujivunia kama ilivyokuwa zaman, vita mauaji na uhalifu leo imekuwa sehemu ya maisha yetu, na chanzo haswa ya yote hayo ni chuki visasi visivyo na suluhu. Na visasi mnapoviweka moyoni huwa kama mzigo ambao unaowatafuna taratibu sio yule tu unaemuwekea visasi bali na wewe mwenyewe, naamini chini ya jua hakuna kosa lisilosameheka( dunia tunapita na vyote tunavyoviona ni starehe ya muda mfupi)ndo mana tukaambiwa tuwe wepesi wa kusamehe sio mara saba tu bali saba mara sabini.
Mwanafalsafa mchina Confucius aliwahi kusema:
“before you embark on a journey of revenge, dig two graves”
TUSIISHI KWA VISASI KILA MTU NI MWEMA KULIKO UNAMVYOFIKIRIA
Nawatakia siku njema wana jamii forum wenzangu wote nawapenda sana