Lady JayDee, Joto Hasira Remix ni poa ila haijashiba kivile!

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Najua wapo wanaopita hapa watakufikishia taarifa.

Nimepata kusikiliza Joto Hasira Remix ambayo umemshirikisha Mkoloni, Songa, na One The Incredible.

Kusema ukweli hii Remix hujaitendea haki kabisa na hao wengine, yaani iko light kimtindo.

Bila kuzunguka, hii remix ingefaa ishirikishe members tuseme wote wa vinega kama kina Soggy, Sugu, Mapacha, Rama D, Suma G, Dani Msimamo, Pin Lawyer, na pengine hao wa sasa kina Songa, Incredible na Mkoloni.

Hii remix ingebamba sana aisee, na Pengine remix kama Mchizi Wangu ingebaki kusoma namba tu.
 
huyu dada anatapa tapa nilidhasema humu kitambo sana.mkoloni,One inc,na yeye wapi na wapi,ushaur mbaya utammaliza huyu.
 
huyu dada anatapa tapa nilidhasema humu kitambo sana.mkoloni,One inc,na yeye wapi na wapi,ushaur mbaya utammaliza huyu.

Wapi na wapi kivipi?
Fafanua.
 
Teh teh teh.......sijaisikiliza hiyo remix ila nshaipenda.
Tupa mawe.....mwaga nyuki
 
ile remix hamna kitu,ile sehemu Prof J anapoanza kuchana kwenye wimbo halisi jamaa wa kwenye remix kapwaya sana
 
Moko wa miujiza(One Inc) anawapa pole walioenda kwenye show mbovu na remix yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…