Lady jaydee kama madonna...

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Wasanii wakongwe wa muziki, nawazungumzia madonna louise veronica ciccone a.k.a MADONNA(USA) na judith wambura mbibo a.k.a LADY JAYDEE(TZ) wameonyesha ukongwe wao kwenye tasnia ya muziki kwa kukaa kwa mda mrefu toka miaka hiyo hadi leo bado wapo kwenye game na bado wanafanya vizuri.
1: Ndio wasanii wakongwe zaidi(waliokaa mda mrefu) kwenye game mpaka sasa ivi.
2:Mbali na changamoto za mastaa wanaokuja kwa kasi marekani kama Rihanna,beyonce,alicia keys na wengine wengi bado madonna anaendelea kuwa juu zaidi yao.kama ilivyo kwa madonna,huku kwetu jide ndiye msanii aliye juu zaidi pamoja na changamoto zilizoletwa na akina lina,recho,dyna na wengine wengi.
3:Madonna ndiye msanii pekee mwenye mafanikio zaidi kuliko wasanii wote marekani, kama ilivyo kwa madonna huku kwetu lady jaydee ndiye msanii mwenye mafanikio kuliko msanii mwingine yeyote tz.
4: Madonna toka mwaka 1982 aanze muziki hadi leo(2013) hajawahi kushuka kiwango, lady jaydee toka mwaka 2000 aanze muziki na yeye hadi leo (2013) hajawahi kushuka kiwango.

Madonna ana miaka 54,huku lady jaydee akiwa na miaka 34 tu, ila hadi leo madonna hajawahi kukabidhi kijiti kwa rihana, hivyo wote wamethibitisha ile misemo ya OLD IS GOLD na ule wa NGO'MBE HAZEEKI MAINI..
 

Ng'ombe hazeeki maini kwa kiingereza wanasemaje,au kila msemo una lugha yake?
 
Kina lina...rachel...wamekuja lkn waapi..hawana jipya sasa...jide z the best kadumu for years...hawa wengine miaka 10 mbele hawatokuwepo kwa game..maana mziki wenyewe wa kubebwa na ruge
 
waendelee tu maana wanaonesha hawaja ingia kwenye game kutokana na kumuiga fulani,bali kwa talanta zao.
 
Umri wake una utata. Kama lady jay dee ana miaka 34 sasa hivi inamaanisha atakuwa amezaliwa 1979, kwa hiyo mwaka 1995 alikuwa ana miaka 16. Niliwahi kusikia mahojiano kati ya prof j na gadna, prof alisema around 1995 jide alikuwa anarap na prof.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…