Lady Jaydee: Mnafiki wa miaka 10, shujaa wa siku 30

Lastname

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
921
Reaction score
297
Na Saleh Ally
MGOGORO wa kimuziki kati yamsanii Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na kituo kimoja cha redio umezidikuchukua kasi huku makundi mawili, kila moja likitengeneza ngome yake nakuamini linachoamini.

Kundi ambalo linamuunga mkonoJaydee na kumuona ni mkombozi, anazungumza kwa niaba yake na wasanii wengine,la pili ni lile linalobaki upande unaoshambuliwa, linatetea ngome yake.

Jaydee anashutumu kubaniwanyimbo zake na kituo hicho ambacho kupitia mitandao kadhaa ya kijamii ameelezawazi kuwa wanambania, wanaziponda lakini hata watangazaji wake wamekuwawakionyesha chuki binafsi dhidi yake.

Jaydee pia aliwaponda wasaniiBen Pol na Linah anayetokea THT kwamba walishindwa kutokea kwenye uzinduzi wavideo ya wimbo wake wa Joto Hasira, kwa madai walizuiwa na bosi wao.


Ujasiri huu wa Jaydee ndiyokitu bora ambacho kimekuwa kikitakiwa kufanyika kutoka kwa wasanii, yaaniwapigane kutetea muziki wa Tanzania hasa kama kuna watu au kundi la watulimejikita katika kuuangamiza.

Lakini ni tofauti kidogo, kwaniwasanii wengi wamekuwa imara na kuwa tayari kujitetea wenyewe tu na si vingine.Nasisitiza mara nyingi, wao ndiyo wahusika wa kwanza na wanapaswa kuanzishamapinduzi kuanzia kwao, mfano kusema naonewa si kitu kibaya lakini je, umewahikupigania wanaoonewa?

Kujitetea pekee unawezakufanya, lakini vipi utafanikiwa kama asilimia kubwa ya kundi la wanamuzikilinaendelea kuonewa. Ukibaki hauonewi pekee na asilimia kubwa ya wasanii auwanamuziki inaonewa, kunaweza kuwa na mapinduzi sahihi?

Ndiyo maana nashangazwa kusikiaJaydee leo anaona ubovu wa kituo hicho, anathubutu kusema hadharani akionyeshawazi ameumia. Lakini miaka 10 au zaidi iliyopita, Jaydee alikuwa kimya nahakuwaza kusema kwamba kituo hicho kinawabania wasanii wengine na ‘kumtukuza’yeye hata kama muziki wake haukuwa wa kiwango kilichokuwa kinazungumzwa.

Siwezi kusema muziki wa Jaydeeni mbaya, nimekuwa kati ya mashabiki wake. Lakini yoyote atanichekesha akisemanyimbo albamu zake zote alizotoa zilikuwa katika kiwango cha juu sana na ndiyomaana leo ni maarufu.

Hakuna asiyejua kwamba miakanenda rudi, wasanii wamekuwa wanaongoza kwa unafiki, kutopendana wenyewe,kugeukana na hata kujenga makundi lukuki, ndiyo maana kila kukicha wamekuwawakishambuliwa maana katika maisha yao hawana umoja.

Jaydee alianza kuwa mtangazajikatika kituo hicho baada ya kuacha kurap, akaamua kuachana na kurap na mwishokuwa msanii wa nyimbo za kubembeleza, mara ya kwanza akianza kutikisa na albamuya Machozi, Solo Thang anaweza kuhadithia vizuri kuhusu hili.

Kuanzia albamu ya Machozi,kituo hicho ndicho kilisimama kuhakikisha anakuwa bora hata kama muziki wakehaukuwa ukimzidi kila mwanadada wakati huo.

Angalia, kulikuwa wasanii kama Stara Thomas,Carola Kinasha ambao kiuwezo walikuwa juu kuliko Jaydee, lakini hawakupewanafasi ya kutosha, badala yake Jaydee ambaye hakuthubutu kuwatetea hata kidogoakaendelea ‘kubebwa’ na watu wakaamini ni bora kuliko yoyote kwa upande waakina dada au kina mama katika kuimba, haikuwa hivyo.

Angalia albamu ya Binti, karibunyimbo zote zilikuwa na ujumbe mmoja, ulikuwa ukimshambulia mwaname mmojaambaye alikuwa amemuumiza Jaydee. Takribani ujumbe wa nyimbo karibu zoteulikuwa ni mmoja, lakini ilibebwa na kuonekana ni moja ya albamu bora kabisakuwahi kuwepo katika muziki wa Tanzania, kitu ambacho hakikuwa sahihi.

Wakati huo wasanii lukukiwalilia kubaniwa, mmoja wao alikuwa ni Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ndiyealimtambulisha mwanadada huyo alipomshirikisha katika wimbo wa Mambo ya Fedha,kabla ya hapo hakuwa na jina. Jaydee hakuwahi kuungana naye hata kidogo hatakwa mstari mmoja wa kumtetea au kuunga mkono kutetea muziki wa Tanzania,kuonyesha anapinga mwenendo wa wanaolazimisha kuwabagua wasanii au kufanyamambo kwa mabavu kwa kuwa wameshika mpini.

Hakuna aliyesikia kilio chaSugu, wasanii wanaochipukia bila ya kujua wasemacho, kisa nyimbo zao zinapigwaredioni, ili kuonyesha shukrani za dhati wakaanza kutangaza Sugu anatapatapa naamekwisha kimuziki!

Ajabu, asilimia kubwa ya manenoyake ndiyo yanayozungumzwa leo, ndiyo yanatumiwa na kila msanii anayebanwa aukuhisi kaonewa. Angalia, hata Jaydee naye ameingia huko! Swali langu hapa je,Jaydee na wengine wanaolalamika, wamekwisha kisanii?

Ndiyo maana nasema, tasnia yamuziki hasa muziki wa kizazi kipya umejaza watu wavivu kufikiri, wenye mioyo ya‘Kichina’, wasio na uwezo wa kuthubutu hata kidogo ambao wanasubiri wayumbe aukuumizwa wao ili wamtafute wa kumuangushia lawama.

Jiulize, kama Jaydee alibebwakwa miaka 10, halafu leo analalamika atakuwa sahihi? Sitaki kumpinga kwa kuwakuna kitu anakiona lakini ninaamini alikiona tokea mapema, akauchuna.

Bado nasisitiza, yeye nawengine wote wanaolia baada ya kuguswa wao nawaita wanafiki, wanapigana kwaajili yao na si kwa muziki wanaoutumikia. Iwapo wangekuwa tayari kupambana kwaajili ya muziki huo, msanii kama Jaydee asingeanza vita leo.

NARUDI KWA JAYDEE
Sijawahi kuingia naye katikamalumbano zaidi ya miaka 10 tokea alipokuwa mwanahabari mwenzangu na sasamsanii. Lakini nathubutu kumueleza kuwa ni kati ya wasanii wasiojali muziki waTanzania na wanajiangalia wao zaidi.

Picha ya unafiki na kujiangaliamwenyewe inaonekana sasa ingawa takribani miaka mitano iliyopita nilianzakuinusa. Leo analia, anabaniwa na anauona moto unaounguza muziki wa Tanzaniaulivyo mkali.

Naamini aliuona miaka kibaonyuma, lakini kwa kuwa alikuwa akitetewa hakuweza kuangalia kwamba rafiki zake,wasanii waliombeba kabla walikuwa wakiungua. Akaendelea kuwapita kwa raha zakemustarehe.

Tungeweza kumuita Jaydee nimpambanaji kama angewakosoa hao anawakosoa sasa katika kipindi walichokuwawamempa mbeleko yeye, basi kweli ingeonekana anapigania muziki wa Tanzania.Sasa anapigania chake tu!

Jaydee amefika mbali kimuziki,alikuwa bora jukwaani na nyimbo kadhaa na nyingi zikapewa ‘over promotion’lakini bado ninaweza kumuita mkongwe. Ajabu alibaki chipukizi hadi leo katikasuala la kutetea haki za wasanii na muziki wenyewe.

Sitaki kumkatisha tamaa kwamapambano aliyoyaanza, ninaamini ana nafasi ya kuanza kuusaidia muziki ambaoumemsaidia. Lakini ndiyo kipindi ambacho anaweza kupata machungu waliyopatawasanii wenzake kunyeshewa mvua na kuunguzwa na jua wakati akiwa kivulini kwa‘msaada’.

Anachokifanya leo Jaydee ninyongeza tu ya walichokifanya Sugu au Afande Sele au wasanii wachache walioamuakuwa wakweli au wale walioamua kuwa wabunifu kama Ambwene Yessaya ‘AY’,aliyekimbia vita ya redio na kuingia katika kurekodi video bora zilizoendeleakumng’arisha.

Simzuii, Jaydee kuendeleakupambana, lakini namuasa anachokifanya kama ni kwa ajili ya muziki akipozwatena, asirudi nyuma.

Ninachomkumbusha, hata yeye amekuwa kundi moja na analowalaumu ambaoangeweza kuwashauri mapema ‘ndani ya mjengo’ kama angekuwa na nia nzuri namuziki wa kizazi kipya. Msisitizo ‘JotoHasira’ liwe la kweli.

 
vip mkuu huu ni walaka,Wosia au tamko,
 
Mnafiki tu huyo. Anaanzisha bifu feki ili auze biashara yake. Sasa hivi eti kuna tisheti za Anaconda zinauzwa. Sasa jiulize, mapato yatokanayo na mauzo yake yanaenda wapi na kwa nani.....
 
Mnafiki tu huyo. Anaanzisha bifu feki ili auze biashara yake. Sasa hivi eti kuna tisheti za Anaconda zinauzwa. Sasa jiulize, mapato yatokanayo na mauzo yake yanaenda wapi na kwa nani.....

kwahiyo kila anaeanzisha biashara ni lazima aseme mapato yake yanaenda wapi.........?
wanafiki ni watu kama nyie
 
Saleh ally utaua the global p.
 
Mnafiki tu huyo. Anaanzisha bifu feki ili auze biashara yake. Sasa hivi eti kuna tisheti za Anaconda zinauzwa. Sasa jiulize, mapato yatokanayo na mauzo yake yanaenda wapi na kwa nani.....

Pesa za matangozo wanazo pata clouds zinakwenda wapi?
 
kwahiyo kila anaeanzisha biashara ni lazima aseme mapato yake yanaenda wapi.........?
wanafiki ni watu kama nyie

Hahaha watu wamezoea kudanganya eti pesa zinaenda vituo vya kulelea watoto yatima.
 
Wewe hujaona, mimi nimeona. Tatizo lako nini sasa?

achana na huyo mwendawazimu atakusumbua.huyo dada ametengeneza bifu,amepata sympasi ya watu na sasa anawatumia kujinufaisha.anatambua wenye chuki zao na clouds media watazinunua sana na yeye atajipatia kipato haramu.jamani kutengeneza brand ikasimama kama ilivyo clouds media inahitaji kujitoa kwa namna zote sasa anakuja kijamba mmoja kwa chuki zake binafsi tu anataka kuiharibu hata kama ni mimi lazima nipambane naye kwa nguvu zote.hawalazimishwi wanajipeleka wenyewe.
 

ukimrefer nani?
 

Kula gwala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…