Lady Judith Listowel mwandishi wa ''The Making of Tanganyika'' (1965) katika nyaraka za Sykes

Lady Judith Listowel mwandishi wa ''The Making of Tanganyika'' (1965) katika nyaraka za Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
LADY JUDITH LISTOWEL MWANDISHI WA ''THE MAKING OF TANGANYIKA'' (1965) KATIKA NYARAKA ZA SYKES

1572754329948.png

Lady Judith Listowel, Ally Sykes amenieleza alikuwa msanii hodari huko Uingereza bingwa wa kucheza dansi na mwanamke mrembo sana.

Akaolewa na William Francis Hare, 5th Earle of Listowel ambae alikuwa Gavana wa mwisho Gold Coast sasa Ghana.

Hapo ndipo ukawa mwisho wa usanii akawa sasa mama wa nyumbani.
Alipata hamu ya kuandika kitabu.

Peter Colmore amenieleza kuwa miaka ile ya yeye ndiye alikuwa kama agent wa Waingereza waliokuwa wanahitaji kufanya lolote Kenya na Afrika ya Mashariki iwe kutalii au biashara na mengine mengi.

Ndipo Listowel alipowasiliana na yeye kumtaarifu kuhusu utafiti wa kitabu hiki.

Colmore agent wake Tanganyika miaka ile alikuwa Ally Sykes rafiki mkubwa wa Julius Nyerere.

Hivi ndivyo Lady Judith Listowel alivyopokelewa na Ally Sykes Dar es Salaam na kufanyiwa ratiba zote za mahojiano na watu wote aliotaka kuwahoji kuhusu historia ya Tanganyika pamoja na Rais Nyerere mwenyewe.

Mtu wa mwisho Listowel kuzungumzanae alikuwa Abdul Sykes.
Hapa pana kitu kaandika Listowel.

Anasema kama angekuwa na muda angepata mengi kutoka kwa Abdul.

Kleist mtoto wa Abdul Sykes akanihadithia kuwa baba yake hakutaka kumweleza Listowel historia ya TANU ambayo Listowel aliitaka sana kuijua.

Sababu ni kuwa mradi wa TANU wa kuandika historia hii mara baada ya uhuru ulipata matatizo na yeye kama mwandishi mkuu alijitoa katika kazi ile.

Laiti tuseme Abdul Sykes kama asingejitoa katika mradi ule wa TANU wa kuandika historia ya TANU leo tusingekuwa na ubishi wa ni ipi historia ya kweli ya TANU au mzozo wa TAA kilikuwa chama cha siasa au chama cha starehe au ni upi mchango wa Mwalimu Nyerere katika uasisi wa TANU au mbona Hamza Mwapachu hayumo katika historia ya TANU ilhali yeye ndiye alikuwa mpangaji mipango na mtàfutaji wa viongozi watakaokuja kuongoza mapambano ya uhuru.

Kwa kuwa Abdul Sykes hakutaka kumweleza Listowel ukweli wa historia ya TANU, Listowel hakuupata ukweli huu na kitabu kikachapwa na upungufu huu.

Ukisoma barua za Listowel alizokuwa akimwandikia Ally Sykes baada ya kukamilisha utafiti na kurejea London utastarehe jinsi anavyoeleza yale yaliyomtia moyo na yale pia yaliyomvunja moyo katika utafiti wake.

Abraham Sykes mtoto wa Ally Sykes alinihadithia kuwa yeye akiwa mtoto ndogo wa kiasi cha miaka minane hivi alikutana na Judith Listowel ofisini kwa baba yake kwenye ofisi yake mjini aliyofungua na Peter Colmore.

Mimi naijua ofisi hii nilipata mara moja kufika pale na baba yangu na kitu ninachokikumbuka siku zote ni viwili.

Kwanza ndipo kwa mara yangu ya kwanza niliona air condition na pili kuona reel to reel tape deck ikipiga muziki mororo.

Hapa ndipo Ally Sykes na Peter Colmore kuanzia mwaka wa 1958 walipokuwa wakitayarisha matangazo ya makampuni makubwa kwa ajili ya High Fidelity Production kampuni ambayo makao yake makuu yalikuwa Government Road Nairobi.

Sasa Listowel akataka kumpa hela Abraham.

Huyu mama pochi yake ya fedha alikuwa anaiweka ndani ya nguo zake za ndani.

Badala ya kwenda pembeni Listowel akakudua gauni lake pale pale kutoa pochi yake.

Bwana Ally akampigia kelele, "Judy you can't do this in front of a child."

Abraham anasema Lady Judith Listowel alicheka akasema, "What can Abraham see I am finished!"

Baada ya miaka mingi nilipata mswada wa kitabu cha Dr. Vedasto Kyaruzi, "The Muhaya Doctor."

Dr. Kyaruzi na Abdul Sykes walichukua uongozi wa TAA 1950.

Dr. Kyaruzi katika mswada wake ameeleza mchango wa Action Group katika mapendekezo ya katiba yaliyowasilishwa kwa Gavan Edward Twining.

Dr. Kyaruzi anaeleza kuwa wajumbe wa Action Group walikuwa Abdul Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Luciano Tsere, John Rupia, Steven Mhando na Hamza Mwapachu akiwa Katibu.

1572779781459.png

Waliosimama kulia ni Dr. Luciano Tsere na mwisho ni Dr. Joseph Mutahangarwa na aliyekaa amepakata mtoto ni Dr. Vedasto Kyaruzi
Ukimsoma Listowel ni kama vile alipewa huu mswada na yeye akanakili kwenye kitabu chake.

Jambo hili limenishtua sana.
Yapo mengi.
 
Andiko zuri sana linachokoza hamu ya kutaka kujua sana kuhusu historia ya Tanganyika.Naamini kabisa katika
 
Back
Top Bottom