>Nini chanzo cha lafudhi?
>Kwanini lafudhi ya watu wa mkoa fulani hutofautiana na mkoa mwingine?ilhali tu nchi moja
Mfano,wamakonde,wachaga,wapemba,wazaramo,wangon, wanalafudhi tofaut kabisa,kwanin,nin tatizo ama tuseme chanzo
Mkuu ndo wewe ninaye kufahamu?Athari ya lugha ya kwanza-au lugha mama ndio hufanya kuwepo na lafudhi mbalimbali. Na tofauti hizi zitaonekana tu pale wazungumzaji wenye lugha mama tofauti wanapozungumza lugha ambayo si yao kwa asili.
Mkuu ndo wewe ninaye kufahamu?
Mimi ndiye...
Aaah! Nakuona u mkongwe huku.
Kitambo sana poti, zamani kilikuwa kisima cha maarifa lakini sasa hivi uhanithi mtupu...
Kwa nini mkuu?
Mambo yasiasa za propaganda yameshika hatamu sana, hii imepelekea watu makini ambao zamani walikuwa wanatoa michango maridadi kulikimbia jukwaa.
Kitaaluma tungesema hivi:>Nini chanzo cha lafudhi?
>Kwanini lafudhi ya watu wa mkoa fulani hutofautiana na mkoa mwingine?ilhali tu nchi moja
Mfano,wamakonde,wachaga,wapemba,wazaramo,wangon, wanalafudhi tofaut kabisa,kwanin,nin tatizo ama tuseme chanzo
Ulimi mama (mother tongue) una nguvu sana, mie hata unilaze Manhatani miaka mia nane, nikiongea lazima ugeuke.
Ndo kabila gani hilo mkuumkolesa
Mi nafikiri hoa ndo wanatakiwa walishape jukwaa, kukimbia inamaanisha wamekubali kushindwa?
Kitaaluma tungesema hivi:
Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira. Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali alikosomea, kiwango chake cha elimu, tabaka lake la kijamii na kadhalika.
Kwa hiyo hapa chanzo kikubwa cha lafudhi ni mazingira alimo huyo mtumiaji lugha, mazingira hayo ni kama yalivyotajwa hapo juu. Lugha mama pia inaweza kuwa chanzo cha lafudhi tofautitofauti, kwa mfano katika kiswahili, hawa watu wakizungumza wazungumzaji wa kiswahili watajua wanatoka mkoa gani au ni kabila gani:
Lafudhi sio kitu kibaya, lakini pia huweza kubadilika kwa kutambua au bila kutambua (hii inaweza kutokea hadi umri wa miaka ishirini na). Lakini chanzo kikubwa cha lafudhi ni mzaingira alimo huyo mzungumzaji.
- Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa
- Amemupiga mutoto ya watu juu amemuibia mfaranga makumi mawili
- Ukikaa nchale, ukichimama nchale
- Wewe unakamuaga mang'ombe tu moja kwa moja
- Mbona unakuwa kinganganizi, nilishakwambia sikupendi lakini wewe bado unaningangania tu!
Ebo! Kwahiyo mnapiga stori kwenye thread ya mwenzenu?Kitambo sana poti, zamani kilikuwa kisima cha maarifa lakini sasa hivi uhanithi mtupu...