Lafudhi

Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira. Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali alikosomea, kiwango chake cha elimu, tabaka lake la kijamii na kadhalika.

Kwa hiyo hapa chanzo kikubwa cha lafudhi ni mazingira alimo huyo mtumiaji lugha, mazingira hayo ni kama yalivyotajwa hapo juu. Lugha mama pia inaweza kuwa chanzo cha lafudhi tofautitofauti, kwa mfano katika kiswahili, hawa watu wakizungumza wazungumzaji wa kiswahili watajua wanatoka mkoa gani au ni kabila gani:


  1. Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa
  2. Amemupiga mutoto ya watu juu amemuibia mfaranga makumi mawili
  3. Ukikaa nchale, ukichimama nchale
  4. Wewe unakamuaga mang’ombe tu moja kwa moja
  5. Mbona unakuwa kinganganizi, nilishakwambia sikupendi lakini wewe bado unaningangania tu!

nakubaliana nawe tukisema chanzo ni lugha mama tunawazungumziaje wamarekani au hzo lugha mama zenyewe zina lafudh hiz lafudh zimetokana na nini hapo pamoja xna
 
ila ikumbukwe lafudhi ya mahali inabadilika taratibu mno kutokana na maingiliano na maendeleo ya elimu
 

Lugha mama ndio chanzo! Lugha moja hadi nyingne hutofautiana sana hasa kupitia sayansi ya lugha (Isimu)..utofaut huo unaweza kuupata katika
1.Idadi ya sauti za irabu
2.Idad ya saut za konsonant..
Hvyo hata ktka matamsh utofaut utakuwepo tu... kwa hapa TZ..katika lugha za makabila yetu mara nyngi lugha yenye matamsh lain huwa na irabu (schwa sound) siijui kswahl tunaiitaje...saut hii ambayo iko katka mfumo wa irab lakn utamkaj wake kifup twawezasema ni mjumuisho wa irabu kuu tano (a,e,i,o,u) na pale itakapotumika kwenye konsonant hutaweza kuickia kama ni a,e,i,o au u. Mfano makabila ya Mikoa ya Arusha+Manyara!
 

katka mazngira ya elimu ni kiwango kiduchu sana mkuu..maana tuna watu wengi sana na degree zao kibao lakin akiongea utajua tu anakotoka!!
 
nakubaliana na usemi kuwa lugha mama ni chanzo ila cjakubaliana nao moja kwa moja tuangalie kuna wabantu ambao lugha zao ni za kawaida si za kukaza na kuna wanaokaza herufi ikiwa wabantu asili yetu moja kwanini tumetofautiana hapa ndo utagundua kuwa mazngira elimu na maingiliano na dunia ya nje. yalianza kuleta mabadiliko ya taratibu kwa watu baada ya miaka mingi na kujikuta lafudhi zao zinakuwa tofauti kabisa. mpaka sasa hizo lafudh za lugha mama zimeendelea kuathiri matamshi yao katika kiswahili chao
 

nakubaliana nawe ila kule wale black american tunajua wametokea africa je kuna muafrica anayezungumza kama mmarekani katika kujifunza kwake kiingereza kwa mara yakwanza jibu ni hapana.
mazingira yamewafanya wazungumze vle maingliano pia yamewafanya hata wazungu wazungumze kama wao,
 

Kwa wale black Amercn ambao wamekulia huko (wakiwa wadogo) ni kawaida sana maana mtoto anauwezo wa kujfunza/kuiga lugha yyte atleast chin ya miaka 6 hv...maana viungo vya utamkaji huwa bado vchanga (havjakomaa/ni lain) ni rahc kushka matamsh yyte kwa urahc na ufasaha tofaut na mimi au wewe!!!
 
Viungo hvyo ni pa1 na
1.midomo(wa juu na wa chin)
2.Ufiz
3. Koromeo
4. Mapaf na vingne huku vikiongozwa na
5. Ulimi
Viungo hv huwa bdo lain sana kipnd cha utoto ni ndo maana mtoto hushka lugha inayomzunguka kwa urahc katka mazingira yake!!
 
nakubaliana nawe tukisema chanzo ni lugha mama tunawazungumziaje wamarekani au hzo lugha mama zenyewe zina lafudh hiz lafudh zimetokana na nini hapo pamoja xna

Kwa wamarekani ni suala jingine, hao tunaweza kusema eneo la kijiografia ndo limechangia (eneo la kijiografia pia ni moja ya sababu za kiisimu katika kutofautiana kwa lafudhi) na ndo maana kiingereza cha Marekani, Uingereza na Australia ni tofauti inagawaje wote lugha yao ya kwanza ni kiingereza, hii inathibitisha eneo la kijiografia kuchangia katika tofauti ya lafudhi.
 
lafudhi hutokana na lugha mama..... kumbuka kiswahili siyo lugha mama kwa kila mtu. mfano. mchaga aliyezaliwa na kukulia Dar, hawezi kuwa na lafudhi sawa na wa kiboro... kibororoni kweli! kwa sababu lugha mama haijamuathiri. kumbuk lugha zinatofautiana. mfano wamakonde hawana 's', wanyaki hawana 'v' nk
 
Lugha mama ina mchango mkubwa sana katika kuathiri lafudhi ya mzungumzaji, Mazingira, maingiliano, sawa kabisa ila hii inajikita zaidi katika lahaja, unachojaribu kukizungumzia hapa mkuu naona ni lahaja na wala sio lafudhi.
 
Lugha mama ina mchango mkubwa sana katika kuathiri lafudhi ya mzungumzaji, Mazingira, maingiliano, sawa kabisa ila hii inajikita zaidi katika lahaja, unachojaribu kukizungumzia hapa mkuu naona ni lahaja na wala sio lafudhi.

lahaja nafaham ni lugha kamili yenye msamiati wake na lafudh just ni jinsi mtu anavyotamka maneno. lafudhi ndani ya kiswahili sanifu inaathiriwa zaidi na lugha mama ila je chanzo cha lafudhi ndani ya hzo lugha mama ni nini hapa ukiangalia kwa umakini utaona ni kama lahaja zilivyozuka ndo vile lafudhi zilizuka
 
Hapo kwenye nyekundu ni 'isimujamii'... Vipi tena mzee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…