Lamborghini waja na V8 Hybrid sportcar: Lamborghini Temerario

Lamborghini waja na V8 Hybrid sportcar: Lamborghini Temerario

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Waitalia hawapoi, wakati juzi juzi tu wametoka kuzindua Lamborghini Revuelto (ipo sokoni kuanzia huu mwaka 2024) iliyomreplace Aventador (iliyotokea 2012 hadi 2023) sasa wamekuja na Temerario itakayoanza kuuzwa 2025 na inamreplace Lamborghini Huracan iliyokua sokoni kutokea 2014.
images (4).jpeg

Kidogo sportcars za Lamborghini zinachanganya kwa muonekano na ata performance, tofauti na makampuni mengine. Ni Lamborghini Urus tu ndio ipo tofauti na Lamborghini zingine kwakua yenyewe ni SUV. Ila for beginners we kumbuka tu hizi sportcars zina series mbili, expensive na less expensive.
lamborghini-temerario-14.jpg

Expensive ndio wakina Aventador ( a vent kwenye door) ambayo kwa muonekano ina bonge la vent kwenye mlango na taa zake zipo kama Y shaped na milango inaenda juu (scissors/suicide doors) wakati milango ya kawaida na taa shape ya W ndio Huracan ambao wana engine ndogo, less power na kidogo cheap.
images (2).jpeg

Sasa tukirudi kwenye Temerario, kwanza imerudisha V8 engine ambayo Lamborghini walishaachana nayo tokea miaka ya 1980s (Jalpa's) na pili ndio turbo charged ya kwanza kutoka kwa Lamborghini.
lamborghini-temerario-engine.jpg

Tukibaki kwenye engine, hii gari ina 4.0L twin-turbo V8 hybrid engine, kujumlisha na electric motors tatu, mbili zikiwa mbele na moja ikiwa nyuma, ambazo jumla zinatoa horsepower 907. Chuma ina top speed ya 343 km/h na acceleration ya 0-100 km/h ndani ya sekunde 2.7!
Temerario_8.jpg

lamborghini-temerario-charging.jpg
Plugin Hybrid system ikiwa na battery la 3.8 kWh, ni sawa na ya kwenye Revuelto kila kitu kasoro vitwist vidogo vidogo mfano hii Temerario ina transmission ya gear 8 lakini haina reverse gear ila reverse yake inachukuliwa na electric motor iliyonyuma.
Lamborghini-Temerario-Interiors-2.jpg

Lamborghini ndani hawanaga mbwembwe sana, ila wako na full equipped cockpit, wao wanasema wamepunguza buttons kwa asilimia kubwa sahivi operations nyingi aniwnkwa touchscreen.
images (5).jpeg

Kuhusu audio system wameshirikiana na watengeneza speaker na earphones kutoka Italy, Sonus Fiber kuweka jumla ya speaker 21 na zaidi katika gari.

Bei ya hii chuma itakua $290,000/= najua hamshindwi.
 
Kudadadekiii....!!!! Dah 2taishia kuziona Kwa picha tu
 
Back
Top Bottom